Haya ndiyo maneno sasa. Akifika hapo Airport kama hana mwenyeji basi yeye aende hata awavae POLISI na watamsaidia kujua jinsi atakavyosafiri kutoka Airport hadi chuoni. Pia anaweza kwenda sehemu za INFORMATION DESK na hapo watampa pia ushauri na jinsi ya kufika huko chuoni.
Mji huo unaonekana uko katikati mwa Geneva na Zurish. Uwezekano hapo ni kufikia Zurich na baadaye au anachukua Train au mabasi ambayo yote unapata hapohapo Airport. Akishafika huko, ndiyo anaweza kuuliza tena achukue Taxi za aina gani za uhakika maana asije akakutana na Wanigeria wa Kizungu au wa kweli na wakamzungusha mji mzima na mwisho wanamwambia alipe shilingi 500.
Asione AIBU au woga kuuliza. Watamsaidia tu ingawa hawa Wafaransa wana ka-ukorofi fulani. Mmoja akikataa kukusaidia, wewe endelea kutafuta mwingine. Asiwaamini sana Wabongo kuwa ndiyo watakatifu na pia asiwatenge watu wa aina nyingine kuwa ni HATARI. Kila mtu amwamini kwa asilimia kadhaa huku akiweka tahadhari kwa kila jambo au mtu anayeongea naye. Mwingine atakuambia ila ukweli amechoka na akachanganya mtaa au eneo. Mwisho unakuja kumchukua kumbe jamaa anasema kweli.
Pia akifika kwenye mji, anunue ramani na aisome. Njia nzuri ninayotumia mie kila ninapokwenda ni kuingia GOOGLE EARTH na kuangalia eneo hilo. Unaweza kwenda hatua kwa hatua hadi kuona Railway Station, umbali hadi chuoni/mtaa atakaoishi, majengo yanaonekana vipi? Ni upande upi wa mji nk na ukiona mtu anakupeleka sehemu sipo, unamuuliza vipi tena. Ndiyo maana Mataxi drive inabidi kuuliza ni CAB gani zinaaminika na ikiwezekana, POLISI akuitie CAB au walinzi wa pale na hapo kuna uhakika kuwa umepelekwa salama.
Nenda na Simu ikiwa na Charge na ukifika Airport, nunua kadi ya simu Pre-Paid na hapo utakuwa na urahisi wa kuwapigia simu chuoni au hata POLISI ukiona umepotea. Kila la kheri.