Mpoki wa EFM aache kukejeli watu.

Efm mtangazaj wa maana n dinnamarios tu
Hivi ile sheria ya utangazaji ya kuwa kila mtangazaji/mwandishi wa habari lazima awe na degree moja itaanza lini vile??kwani ndio utakuwa mwisho wa hao eti ana kipaji cha utangazaji tu!!kina zembwera,kocha mchezaji,mzee wa unatema kushoto unafukia kulia(mbwiga),umri wa kustafu yeye ndio anaajiriwa!!
 
Haa haa haa hyo Sheria ikipitishwa
Ujue xxl na clouds kwa ujumla tunawaambia rest in peace
 
Asidharau watu, Kama ndo hivo nitafuta comedy zote.
 
Haa haa haa hyo Sheria ikipitishwa
Ujue xxl na clouds kwa ujumla tunawaambia rest in peace
Nakumbuka kuwa walipewa miaka mitano ya kujiendeleza!!kama sijakosea tunaenda mwaka wa tatu au wa pili!!,hapo patamu mtu ana zero form four,upewe miaka mitano uwe umepata gamba la degree si hatari hiyo?!!mbona wengi watarudi kwenye fani zao za kuchekesha.
 
Kwa sasa wapo TV gani? maana nilisikia tangu watoke tbc wameachana na comedy.
 
Mpoki Form 6 nadhani. Ila si unajua form 4 na 6 za siku hizi. Walimu vimeo wanafunzi vituko..... Ila Mpoki akitulia akili zake ni nzuri zaidi ya wenye degrees wengi tu. Sema hizo kejeli bwana... Tunakukosoa Mpoki kwa sababu tunakupenda..
Form 4/6 ya siku hizi?Unaongelea miaka ipi mpoki amerudi shule?

Yule ni la 7 mkuu.
 
Sioni kama ni kejeli hiyo tunaita "GET ANGRY,BE INSPIRED,IT CAN BE YOU" Kitendo cha kusema inakuwaje una 50 bado unapanga? Ni kweli bwana yaani una 50 years bado unapanga? wewe unaona sawa? Ingawa anaongea kicomedy lakini huwa mie namuelewa sana,tuchukulie kama challenge,anafanya kusudi kukutia hasira ili uongeze juhudi za kusaka mapene.
 
Wachora mstari kati ya komedi na maisha,wakati ile ni sanaa sehemu ya maisha.
 
Alia


Alianza vizuri sana Mpoki pale EFM. Akichekesha na kuelimisha....Sijui kimempata nini hivi karibuni. Au kalewa madili.... ya hela za matangazooo....? Unajua binadamu akipata matako hulia bwataaa... Easy Mpoki.. Easy....

Mpoki asije akaukejeli hata msiba wa Mzee Majuto leo. Maana sijui kimemkuta nini siku hizi anakejeli sana watu. Hajali umri wala hali ya mtu.
 

Changamoto ni kwamba hata hao waandishi na watangazaji wenye shahada baadhi yao ni vilaza zaidi.
Vyeti havifanyi kazi kid. Na wengine hivyo vyeti wameghushi. Akina Mpoki sio watangazaji kiviiilee. Ni mchekeshaji na sina tatizo na elimu yake. Ila aache kejeli na sanifu kwa Watanzania....
 
Mpoki Form 6 nadhani. Ila si unajua form 4 na 6 za siku hizi. Walimu vimeo wanafunzi vituko..... Ila Mpoki akitulia akili zake ni nzuri zaidi ya wenye degrees wengi tu. Sema hizo kejeli bwana... Tunakukosoa Mpoki kwa sababu tunakupenda..
Aisee bongo nyoso. Form 6 anamiliki nyumba na prado jipya na pamba kali
Kweli phd sio kutoboa kimaisha
 
Mpoki asije akaukejeli hata msiba wa Mzee Majuto leo. Maana sijui kimemkuta nini siku hizi anakejeli sana watu. Hajali umri wala hali ya mtu.
Tayari mbona.kamkejeli steve
 
Mkuu nakushauri ubadili mindset kwanza. Kwahivo unaamini kwamba umedharauliwa au we ni masikini. Basi fanya kweli muoneshe mpoki kwamba we siyo maskini kwa kutengeneza mkwanja mrefu.
Acha kulialia mkuu pambana tu nawe utakula kuku kwa mrija.
Ukiwa mtu kuwaza kudharauliwa basi hakuna atakayekuonea huruma duniani utabaki na stress zako
 
Eti chumba kimojaa na mandoo mikaa mavyombo kibao kwenye korido ndicho anachokandiaga..... Nani anapenda kuishi hivyo... Si basi tu. Nchi Haina mipango mizuri. Nchi zilizoendelea nyumba hazijengwi na individuals.
Ile jokes tu mkuu kutokana na hali halisi ya maisha ya kila siku ya Watanzania walio wengi (anapotoa kitu kama kile kila akijaangalia nyumbani kwake anaona aisee kweli kifuatacho ni kicheko na ukimwangalia mwenzako na kicheko kinazidi)...mie kwangu hapo kuna funzo kwamba unapo plan kujenga nyumba yako hakikisha kwamba ina stoo kubwa
 
Yaani hapa ndio tunashida kwa wengi wetu tusionacho...wakati mwingine unakasirika tu ukimwona mtu anatembea huku anakunywa juice ya kopo kwa kumwona kama anajidai wakati huohuo anaekula miwa na karanga huku anachafua mazingira unaona kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…