Lazaro anatafuta chep publicity.....hana lolote arudishe pesa zetu za summer camp.
Nimefanikiwa kupata kujua alichoongea Lazaro...
Kimsingi walitoka nje ya mada. Mada yenyewe ilikuwa inaongelea vinasaba vya DNA lakini wakajikuta wanafikia huko kwenye issue ya mishahara ya wabunge, suala la nyaraka za serikali etc.
Ninachoweza kusema ni hivi: Lazaro alivyoongea alionekana anaongea kwa dharau sana as if anawa-under estimate watanzania wanaoangalia. Halafu alionekana kuwa mtu wa kuamini upinzani ni sawa na u-mbumbumbu.
Binafsi nafurahishwa na uwepo wa upinzani na najua hilo tunaweza kutofautiana na Lazaro. Madai kuwa wapinzani wanakumbatia issue ya EPA na BoT kuwa yao na kudai ni ya CCM naona ni kuendekeza siasa badala ya kuangalia maslahi ya taifa.
Endapo wapinzani ni kweli wanakumbatia mambo haya na kudai ni yao basi nao watakuwa wameishiwa, kinachotakiwa katika suala hili ni kukubaliana kuwa tumefanikiwa kuwajua wabaya wetu ingawa wengine wameendelea kubebwa 'live'. Ukweli ni kwamba iwe ni CAG, CCM au Upinzani ndio uliibua issues hizi bado inabakia kuwa zile zilihesabika kuwa nyaraka za serikali na haikuwa rahisi nyaraka hizo kuwekwa hadharani na uwezekano wa reports hizo kufanyiwa kazi ulikuwa mdogo! Alichoongea Dr. Slaa katika hili yuko sahihi, waliofichua uozo huu wanastahili kupongezwa badala ya kuwabana au kuanza kutafuta sheria za kuwabana kuhakikisha wanaharibiwa maisha!
Suala la mishahara ya wabunge naona Lazaro bado alikuwa katika kitu kilekile ninachopingana nacho, kudai kuwa Dr. Slaa anatafuta umaarufu kwa kuwachochea wananchi bure.
Alichoongea Lazaro kuwa ndiyo mipango ya serikali katika kuwaokoa watanzania ni hadithi za siku nyingi ambazo bila kelele za watu kama Dr. Slaa and the like tutaendelea kuzisikia hadithi hizo.
Nasikitika kuwa Dr. Slaa huenda alielemewa maana inaelekea hata watangazaji wenyewe wako biased sana.
Tumeandika humu, yameandikwa magazetini na kwingine kwingi... Tanzania imezidi kuwa na matabaka, tuchukieni kwa kusema hivi lakini hatuwezi kuukwepa ukweli huu. Alichokisema Dr. Slaa kina ukweli mkubwa ingawa kama alivyoonekana kutahadharisha Lazaro inawezekana kabisa mtu kutumia kauli kama hizo kuufanya umma uione serikali kuwa haiufikirii na hivyo jamii ya chini kuamua kufanya kitu ambacho kinaweza kupelekea serikali iliyo madarakani kupoteza fursa hiyo!
Ukweli unabakia palepale kuwa Dr. Slaa na Lazaro wanaishi katika Jamii ambayo ina matumizi sawa na wao... Vyakula mnavyokula ni vya aina moja tu japo manjonjo ya makaangizo yanaweza kuwatofautisha, barabara mnazotumia ni zilezile, mafuta kwenye magari mnaweka sawa na raia wa kawaida, hata vituo vya televisheni mnavyoangalia ni vilevile! Haina sababu ya kuendelea kuangalia hii hali ikiendelea, kelele zitapigwa, iwe zinaonekana za vyura ama za wenye uchu wa madaraka lakini hazitaisha katika hili. Mtanzania anateseka sana ndani ya nchi yake!
Katika suala la nyaraka napenda kumfahamisha Lazaro kuwa sisi watanzania tuna mapenzi na taifa letu! Tunalipenda kiasi ambacho hatuko tayari kuona linaaibishwa kwa namna yoyote ile. Namhakikishia hata akiitembelea JF (au kama ni member) anaweza kuthibitisha kuwa mara zote tunawapa tahadhari juu ya mambo ambayo yanaelekea yanahatarisha usalama wa taifa letu. Nawashukuru policy makers wa Tanzania ambao walionelea ni vema wakimtambulisha mtu wao hapa JF na kuwa anatufahamisha pale anapoona kuna sehemu inalivua nguo taifa tukachukua hatua, hawa wanaangalia taifa na si chama!
Lazaro, unaweza kuwa sahihi katika mengi lakini katika mengi pia hauko sahihi!
Invisible