Mahakama kuu ya TZ leo imefutilia mbali masharti ya dhamana ya Amatus Liyumba wa BOT iliyokuwa imetolewa na mahakama ya hakimu mkazi wa Kisutu na kuweka masharti mapya pia kuamuru kesi hiyo ipangiwe hakimu mwingine.
Sasa Liyumba pamoja na masharti mengine atatakiwa kuweka dhamana ya nusu ya hasara ya kiwango cha pesa anazotuhumiwa kuisababishia serikali ambayo ni Bilioni 221, HIVYO DHAMANA YAKE NI ZAIDI YA BILIONI 110,
Jamani hata kama mtu anatuhumiwa ufisadi, dhamana ni haki yake! inaonekana kweli kuna mkono wa mtu nyuma ya kesi hii...Yaani dhamana ya mabilioni ya shilingi!! Ukomaliaji huu wa serikali ungekuwa unafanywa pia kwa kina Rostam nadhani mambo yangekuwa safi sana!
Afadhali yeye bado anaishi, kuna watoto na wanawake ambao wanakufa shauri ya kukosa dawa. Laiti mabilioni waliyokuwa wanajichotea yangetumika ipasavyo nchi yetu isingelikuwa hapo ilipo.
Japo yeye ni dagaa tu katika nchi ya Manyangumi na Mapapa lakini za mwizi ni arobaini ya yakikukuta usilalamike.
Ningependa kuuliza , hivi imeshawahi kutokea kwa mahakimu kutolewa/kuondoka katika kusikiliza kesi zaidi ya mara moja within a period of meizi sita?
Hawa mahakimu wanaodoka kwa shinikizo au rushwa au kutokubali pressures kutoka juu?
Kwa maoni yangu binafsi PCCB/DPP hawakuwa makini wakati wakifungua hii kesi. Wana jaribu kuonyesha kana kwamba Liyumba anapata dhamana kwa njia isiyo halali.
Wampe hiyo dhamana na waendeshe hiyo kesi haraka na ufanisi na waprove within reasonable doubt kama Liyumba ni guility.
Tutaanza kusikia kuwa uchunguzi haujakamilika!
Tanzanian law is a joke! lakini sijui wanatumia vifungu gani kujustify haya wanayoyafanyaThat law is impractical and essentially unfair..
tuache mkonoono wa sheria ufanye kazi yake...sisi ni watazamaji tu na mashabiki...
mwisho wa yote lazima UKWELI UJULIKANE ...LAZIMA..AWE AMESHINDA YEYE AU AMESHINDWA...JUST WAIT..SOONER RATHER THAN LATER MAJIBU YATATOKA...
Mbona akina Mramba walilegezewa na wanapeta uswazi?
Akina Jeetu Patel walilegezewa na wengineo wapo uswazi huyu Liyumba naona kuna kamkono ka mtu kamekaza pale....tuseme yeye peke yake ndo kaitia hasara serikali kwenye majengo hayo? Mbona Bodi nzima wapo uswazi wanapeta tu?
ndio hapo!
Ochu, Chaku na Kinyamis, muwe mnasoma thread nyingine kwanza.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/31387-mpya-liyumba-akwama-tena-mahakamani.html