Mr Bean: Mhandisi anayezeekea kwenye vichekesho

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Inawezekana kuonekana ni jambo la ajabu kwa mtu mwenye taaluma inayoheshimika katika jamii kutojihusisha kabisa na kazi hiyo, badala yake kufanya kitu asicho na msingi nacho.

Wengi huamini kuwa taaluma zinazopatikana darasani ndizo zinazopaswa kuwa mwongozo wa maisha yetu, hivyo baada ya kuhitimu ni lazima kufanya shughuli zinazofuata mwongozo huo.

Ukweli ni kwamba inawezekana kabisa ukawa na taaluma uliyoipata drasani, lakini usiifanyie kazi, badala yake ukajihusisha na kitu kingine tofauti lakini ukafanikiwa kufanya vizuri zaidi kuliko upande wa taaluma yako.

Hilo limedhihirishwa na mkongwe wa vichekesho Rowan Atkinson, ambaye anafahamika na wengi Mr Bean. Licha ya kubobea katika fani hiyo ya uchekeshaji, kitaaluma Mr Bean ni mhandisi wa umeme.

Licha ya ndoto yake ya kuwa mhandisi wa umeme na kufanikiwa kuipata taaluma hiyo inayohitajika wakati wote katika jamii Mr Bean, hajawahi kufanya kazi inayohusiana na umeme, badala yake amehamishia mapenzi yake kwenye fani ya vichekesho.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Daily Telegraph la Uingereza, Mr Bean ameeleza kuwa alikuwa akipenda zaidi sana hesabu na kutamani siku moja angekuwa mhandisi hali iliyofanya kutilia mkazo masomo yake hadi alipopata nafasi ya kusoma katika Chuo Kikuu cha Newcastle na kufanikiwa kuhitimu Shahada ya Kwanza katika uhandisi wa umeme.

Baada ya kuhitimu shahada hiyo alijiunga na Chuo Kikuu cha The Queens College Oxford kwa ajili ya Shahada ya Uzamili katika fani hiyohiyo ya umeme na alipokuwa chuoni hapo, ndipo alipoanza kujihusisha na masuala ya sanaa, baada ya kuteuliwa kumsaidia Richard Curtis aliyekuwa mtunzi na mchekeshaji wa jukwaani.

Taratibu Mr Bean akaanza kupata uzoefu, hatimaye akafanikiwa kuandika na kucheza mfululizo wa kichekesho chake cha kwanza kilichofahamika kwa jina la ‘Not the Nine O’clock.’

Kutokana na uwezo mkubwa alioonyesha katika kazi hiyo, Mr Bean alianza kukubalika katika ulimwengu wa vichekesho, hata alipomaliza chuo aliamua kujikita zaidi katika fani hiyo.

Aina yake ya uchekeshaji bila kuongea imemfanya kuwa miongoni mwa wachekeshaji mashuhuri duniani na kuweka rekodi ambayo mpaka sasa haijavunjwa na mchekeshaji yeyote.

Baada ya umri wake kusonga mbele, mwaka 2012 Atkinson aliweka wazi kuacha kucheza uhusika wa Mr Bean uliokuwa ukimtaka kufanya vitu vingi vya kitoto.

“Licha ya uwezo wa mtu mwenye umri kama wangu kuanza kupungua, nahisi pia kuigiza kama mtoto hakunifai tena,hata kama nitalazimika kufanya, haitakuwa kama awali,”aliliambia Daily Telegraph.
 
Cheki hii ya mwaka 2011 - "Johnny English 2- Reborn"
 
Arsene wenger nae ni mhandisi wa Umeme, kaweka kando kaingia mpirani
 
Bean yupo juu kwenye uchekeshaji..
Uhandisi asahau tuu
 
wenger ana degree ya uhandisi vile vile
allipatia chuo gani?mimi navyofahamu ana degree ya uchumi aliipatia universty of strasbourg,na pia ana diploma ya ualimu wa soccer
 
Hiyo Ndio power of Destiny. Hamna ubishi hapo,mfano mzuri ni wewe mwenyewe.
 
Mr.Bean noomaa yaan hayupo anaemfikiaaa kuchekesha huyu jamaa yaan hata kama umenunaaje ukiangalia vichekesho vyakee hoii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…