Mr. Blue acha kujikweza

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Mr Blue wa siku hizi sio yule wa miaka ile.

Siku hizi jamaa kabadilika sana yani anajisikia kweli mpaka anaboa.

Hivi ni nani anamdanganya huyu jamaa kwamba na yeye ni staa hapa TZ? Hivi tukisema tupange listi ya mastaa Mr Blue naye atatoka? Si itakuwa ajabu la mwaka hilo.

Miaka ya nyuma jamaa alikuwa homie sana yani haringi wala nini halafu hajikwezi ila siku hizi doooooh anaboa,imefika pahala ananata mpaka kwa mastaa wenzake.

Mwanzoni Insta alikuwa amewafollow mastaa wengi tu (2K+)ila siku hizi baada ya kuota mapembe kawa unfollow wote amebakisha 31 tu na hakuna staa hata mmoja wa kibongo.

Ameamua kum unfollow mpaka Diamond Platnumz na crew nzima ya wasafi .

Kwa mwendo huu jamaa atazidi kupotea.
 
Jamaa kila Siku nakwambia kuna haja ya wewe kucheki jinsia yako vizuri,asubuhi yote hii bado watu tuna kauchovu cha mechi ya asubuhi mwenzetu umekurupuka kama kawaida yako umeanzisha thread ya kikuda,hii inaonyesha kwamba umelala usiku mzima ukimuwaza khery sameer na chuki zako zisizo za msingi,kisa tu hakuwafollow mabwana zako wa WCB basi umeona uje utudekee humu,unampangia maisha wewe ni mke wake?,unamnunulia bando??,unajua interest zake!? Huu ni uchawi wa kike kabisa ndugu yangu
 
Kumlazimisha mtu kufollow mastaa ni UMAMA
 
Nani aliyekwambia WCB ndio baba wa bongo fleva.. eti bila wao huwezi kutoboa?
Blue pale wasafi kuna mtu wa kumtoa kwenye jukwaa?.. au ww unasema blue gani?,
Ukinyimwa pesa na msanii unamkunjia ndita, ukipewa unamkimbizia mwenge humu had kuche.
 
hakuna mtuu star kama mr blue acha unafiki uende mbinguni mtu star tangu noti ya elfu kumi ni ya rangi ya blue wewe utakuwa mzee wa mateam hakuna star kama huyo jamaa
 
Hivi kwani Diamond kawafollow mastaa wrote wa bongo?
 
We jamaa unaongea kinyume,wakitajwa mastaa mr blue lazma atoke,acha kuwa unfollow jay-z hana hata hiyo account na ni superstar,usimpangie mtu maisha wewe
 
Hizi chuki zingie bhana! Hivi asingekuwa staa ungeandika uzi kumhusu kwenye hili Jukwaa la Celebrities? Halafu wewe ni nani kumpangia mtu watu wa kuwa-follow?...
 
Hizi chuki zingie bhana! Hivi asingekuwa staa ungeandika uzi kumhusu kwenye hili Jukwaa la Celebrities? Halafu wewe ni nani kumpangia mtu watu wa kuwa-follow?...
Mkuu huyu ni mke wake na Mr blue so mwache ampangie tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…