Mr Ibu kuzikwa leo

Mr Ibu kuzikwa leo

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766

download.jpeg

Marehemu mwigizaji kutoka nchini John Okafor (62) maarufu Mr Ibu anatarajia kuzikwa leo Juni 28, 2024 katika mji aliozaliwa wa Amuri, Jimbo la Enugu.​

Mr Ibu alifariki dunia Machi 2, 2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Evercare iliyopo nchini Nigeria ikiwa ni siku 118 toka alipofariki.

Kifo cha mwigizaji huyo kilitokana na matatizo yaliyotokana na kukatwa kwa moja ya miguu yake.
 
Jamani sa muda wote huo ni wanakaa kuombolezaaa??? Au wanaendelea na mambo mengine?
 
Mila za ovyo kweli,siku zote hizo mnamtesa mtu kwenye mafriji
 
Wamenikumbusha shika neno tenda neno.nabii wao alipokufa waliamini angefufuka.weee
 
Wamenikumbusha shika neno tenda neno.nabii wao alipokufa waliamini angefufuka.weee
Aisee umenikumbusha kitu cha zamani kidogo,
Bwana yule alitusababishia msiba ,
Nakumbuka baba yangu mkubwa alikia anasali kwake,
Basi akaja kupata magonjwa ya utu uzima sukari ,presha ndipo madaktari wakashauri kuwa kuna baadhi ya vyakula mzee asiguse ,
Nabii bwana alipojua akapiga marufuku

Na kumwambia mzee kula kila kitu hiyo mifuta futa usile kunywa kabisaa ,sijui chumvi weka mpaka kwenye kahawa yani tafrani mzee hakuchukua round akaishia
 
Dah poleni .walimuweka mapinga kule wakajua atafufuka.akaanza kubadilika wakaona isiwe tabu wakamzika
 
Tanzania tumewakilishwa na nani kwenye mazishi? Nadhani waziri wa utamadini angejiongeza kupelekwa rambirambi za wa bongo. Huyu Mwamba kaongezea watu Sana umri wa kuishi kupitia vituko vyake yeye na SAM LOKOLOKO na UMUSOFIA
 
Back
Top Bottom