Mr. Kuku kuanza tena biashara

Mr. Kuku kuanza tena biashara

Peasant educator

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2020
Posts
209
Reaction score
187
Habari wadau.

Mwaka jana kulikuwa na taharuki juu ya uendeshwaji ya biashara ya Mr. Kuku mpaka kupelekea kushtakiwa kwa kosa la upatu na kupelekea wawekezaji wengi kupoteza fedha zao.

Mwisho wa kesi ile ilikuwa ni kutaifisha fedha za mr. Kuku zilizoshikiliwa na serekali na kumtoza faini ya million kadhaa.
Sasa, mr. Kuku amerejea na ile biashara na kufuatia agizo la DPP juu ya upatu nk. Ningependa nielewe nini kimebadilika kwenye ule uendeshwaji wa ile biashara maana Mr. Kuku imerejesha ule uwekezaji.

Msinichukulie vibaya mie sio chawa jamani. Wameweka limited comments insta alafu ukiwasiliana nao lazima uende Kigamboni wakati watu tunataka taarifa tu ili tusije kufilisiwa tena na kujikuta matatizoni na utawala.

Return zao kwa kweli ni nzuri na kuridhisha ila salama wa fedha na investment upo. Nini kimebadilika sasaivi? Naomba mtueleweshe!!!
 
Atakua amepewa vigezo na masharti na anavitekeleza
 
Amebadili mfumo sasa hivi anatumia mfumo wa kukodisha vitalu vya kufugia
Kama nimekuelewa, ina maana say kitalu x chenye mabanda wawili unaweza kumlipa kodi ya mwaka mmoja. Baada ya hapo ukifuga au usifuge kazi kwako lakini mwaka ukiisha anakuja kuchukua kod yake tena; yaani kama tunavyofanya fremu za biashara; au?
 
Back
Top Bottom