Mimi ni member mpya wa JF, hongereni kwa maoni. Kwa leo kilichonigusa ni hii issue ya kusema kuwa yanayotokea Zimbabwe, yaliyotokea Kenya na Somalia na Dafour ni aibu kwa Afrika, jamani hee!! Haya maufisadi ya Tanzania sio aibu mbona hamkuyataja? Kwamba ni aibu kwa Tanzania na Afrika! Eti ni nchi ya amani na mfano wa kuigwa! Amani wapi wakati watu wanachukua mabilioni ya pesa halafu wanaviita eti vijisenti. Kwa hiyo inatakiwa huyo mheshimiwa aje amalize kwanza hili lililopo hapa nyumbani, hayo ya Zimbabwe atayatolea tamko akiwa hapa nyumba na hata akiyatolea tamko huko hayatuhusu ki-hivvo bwana Zimbabwe ni sehemu ya Afrika. Hivi baba unaweza kwenda nyumba ya jirani kusuluhisha mgogoro wa kifamilia wakati kwako kunawaka moto, ni sawa na kusema mtoto wa mwenzako kashindikana wakati wakwako ndio hafai hata kutizamwa.