Mr Price wanafungasha virago, yamewashinda?

Mr Price wanafungasha virago, yamewashinda?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu Mr. Price yamewashinda kwa mara nyingine tena, wanafunga duka moja kwa moja.

Pia soma: Nakumat yainunua Shoprite Tanzania

Mazingira ya biashara bongo ni magumu sana au wenyewe ndio ndio wazinguaji?

Ilianza Shoprite wakabwaga manyanga, Game ikaangukia pua na sasa Mr. Price wamebwanga manyanga!
 
Tazama ramani utaona nchi nzuri, yenye mito na mabonde mengi ya nafakaaa.
 
Tuna little More... lazima wabwage manyanga

Mchina kariakoo yupo, kila eneo ameenea! Mkandarasi yeye, madini yupo, tech yupo

Kwa ufupi anatafuta pesaaa
 
dah hao Nakumat hawana products zuri na chaguo pana kama mr Price.
 
Vitu viwili vinachangia hizi biashara za supermarket kufa

1. Tumeshazoea viduka vya mangi vya mtaani kwetu tena vingine vina daftari la mkopo.

2. Hali ya kiuchumi ya mtu moja moja haiwapi watu fursa ya kwenda supermarket budget zetu wengi na hand to mouth...
 
Wabongo wengi hali zetu za kiuchumi ni walewale tu.

Hizo supermarket ni biashara za nchi ambazo wananchi wake wana purchase power kubwa pia nchi inakuwa na mfumo maalum wa kuuza bidhaa mfano bidhaa zinakuwa zinapatikana kwenye supermarket tu, sasa huku Tanzania maduka ya mangi kibao, mini supermarket kila kona, masoko mjinga lundo, nani ataenda kwenye hizo supermarket kununua zaidi ya wale wachache wenye uwezo plus slay queens na masharobaro ambao wanakaa supermarket masaa mawili ila ananunua ice cream ya jero tu huku kwenye gallery yake keshapiga picha 70+ za kwenda kuringishia.

Kifupi ni kuwa wabongo maisha mazuri tunaigiza hatuyaishi
 
Purchasing power ikiwa chini sana, utamaduni wa kununua vitu in bulk ukiwa haupo, biashara ya supermarket inakosa wateja.
 
Wakuu Mr. Price yamewashinda kwa mara nyingine tena, wanafunga duka moja kwa moja.

Pia soma: Nakumat yainunua Shoprite Tanzania

Mazingira ya biashara bongo ni magumu sana au wenyewe ndio ndio wazinguaji?

Ilianza Shoprite wakabwaga manyanga, Game ikaangukia pua na sasa Mr. Price wamebwanga manyanga!
Watanzania hawana utamaduni wa kununua vitu supermarket wakidhani bei ni kubwa wakati siyo kweli ndo maana supermarket kubwa huwa hazitoboi bongo
 
Mkuu Mchele wa Mbeya Supermarket ni bei rahisi kuliko mitaani ? Au Dawa ya Meno sabuni za kuogea ni bei chini kuliko Tandale, Manzese,mwananyamala, Tandika na Buza.
 
Ina maana nyomi lote linaloenda hapo mlimani City hawafanyi shopping, au watu wengi wanaishia kupiga selfie tu no kununua

Ova
 
Back
Top Bottom