Elections 2010 Mr. Sugu ashinda kura za maoni ubunge CHADEMA - Mbeya mjini


Kwani sugu kafanya muziki tu? Hata huko katika muziki hamna opportunities za kuonyesha leadrship skills? Si tayari tunaona watu wanaeleza alivyoshikia swala la hakimiliki bango?

Leader anajulikana popote pale. Tatizo mtu ukiuliza wanaomjua watoe habari unaonekana kama unataka kumchimba.

Mimi binafsi ningependa kuona watu kama Sugu wanaingia mjengoni, yule anaweza kuleta matumaini kwamba kufokeana na status quo ataweza, culture nzima ya Hip Hop iko katika kubishana na status quo.

Kikwete kupita bila kuwa vetted ni tatizo tulilofanya, sasa tusirudie kufanya kosa hilo tena. Two wrongs do not make a right.Ukikosea mwanzo, kosa la mwanzo halihalalishi kurudia kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…