Mr Ttouchez: Nikipata tatizo lolote mhusika Chidi Benz

Comment za Wana JF wengi inaonesha ni kiasi gani JF imejaa Wahuni.

Ni ngumu sana kupambana na Mtu ambaye wewe wala huwezi kuona au kutaka kumsababishia madhara mabaya au hata kifo, ingekuwa unapambana na Mtu Mstaarabu ambaye mkibadilishana ngumi mbili tatu mambo yataishia hapo...lakini Mtu kama Chidi stori zake zinajulikana...wale si aina ya Mtu wa kumpuuza kirahisi.

Wewe jiulize kwa nini Jamii ya Wamarekani Weusi kuna visa vingi vya kuuwana kwa risasi?...hamuoni ya kwamba hali ingekuwa hivyo hivyo hata huku kwetu kama bastola zingekuwa zinapatikana kirahisi?.
 
Kupambana na teja lazima ujihami.

Aisee hao watu achana nao kabisa anaweza kukukita bisibisi au kisu halafu yeye asione tabu kabisa anabembea zake kama kuku mwenye mdondo.

Mimi namsifu jamaa kutoa tahadhari hii Haina maana yeye hawezi pambans kiungwana na kihuni

Uwezo anao ila lazima aandae mazingira Incase child akiendelea kuwa tishio kwake, mazingira yampe favor.

Kama ushapita kule mchikidown kariakoo ukaeaona mateja walivyojaa utakuwa unaelewa jamaa wanajiamini kupita maelezo ila nguvu Hana Sasa jichanganye upige ngumi ... [emoji2]
 
Jamaa katumia busara sana, inaonekana ni mtu anayeifikiria kesho yake. Halafu hayo maugomvi hayajawahi kuleta faida hata mara moja mwisho wake huwa ni kuuana tu na kuanza kusumbùa watu rambirambi kwa mambo ya kipuuzi

Pia hii tabia ipo sana siku hizi, kuna watu wanaamini kuwa ukiwa na kazi, biashara, kipato n.k basi pesa ipo tu / huna matumizi nayo, ukimwambia sina anakuchukia na kukuchukia, wabongo tuna safari ndefu sana
 
Ni kweli mkuu, jamaa ametumia busara kujihami kijanja maana mtu mwenye Akili timamu,mwenye majukumu na mwenye kutaka kuona kesho yako inakuaje hawezi kuwa na bifu na Teja ambae yeye hataki kujua kesho yake itakuaje na wala hana cha kupoteza

Yani ni mara elfu moja uwe na bifu na mtu yoyote yule Duniani ila sio Teja, maana swala la utimamu wa Afya kwako linakuwa majaribuni muda wote hadi muda wa kulala ndio unapata Amani ila kukikucha tu maisha ya hofu tena yanarudi

Kweli kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wasiotaka kufanya kazi na wamegeuza kuomba omba ndio kazi rasmi na kama usipompa inageuka bifu kama ilivokuwa Kwa cheed

ila kutokana na maneno hayo ya touch mwenyewe inawezekana Katika kujibishana na cheed jamaa alisema maneno yaliyomuuma cheed na wala sio matusi Bali maneno ya ukweli ambayo yanamuhusu cheed

Maana hakuna kitu kinauma kama ukweli, hawa ma producers ndio wanayajua vizuri maisha ya wasanii ambao wamepigika maana wao ndio walikuwa wanashinda nao studio kipindi wapo juu, kwahiyo wanajua story zao kibao wakati wapo on top

Cheed anajulikana ni mkorofi miaka yote na ni kweli siku hizi anaomba sana hela kwa jamaa zake wa zmaani ikiwepo wasanii pia, ila sio wa kufikia hatua kama hii ya kuanza kuwinda mtu ni lazima bwana touch alimtamkia maneno yakapiga kwenye mshono sasa Mwamba imemuuma

Kwa maisha ya Teja kukutoa uhai kwa kitu asichokijua ni dakika 0 tu, wao waga hawaulizi kafanya nini bali swali waga oya nikimaliza kazi nakukuta wapi unipe changu? Sasa touch kawa mjanja japo wapo watamuona mshamba, kaona heri akimbilie kwenye jamii ambayo itamkemea cheed na hatimae hii issue iishe kama haikuwepo vile
 
Mara ya mwisho ninemuona Benzino naye akimsagia hayati Kunguni....
 
Wanasikitisha sana watu wazima kuanza kuwindana kisa elfu 50.. wakae tu wayamalize maisha yaendelee
 
Hi mbaya sana anaweza akatokea mtu mwingine akakudhuru na hatimaye akili ya yako itakupeleka kuwa ni Chid
 
Haha jamaa anajikuta gangster from The Bronx
 
Touch kaingia Dar ashakuwa mtu mzima na akili zake akitokea songea

Na hii mambo ya kuonesheana umwamba kwa vitu ambavyo navina hela ni upuuzi tu

If doesn't make money, it doesn't make sense mzee
Fact.
 
50,000 apewe hivi hivi?Amtegee tundu hilo asulubiwe then akaimalze hio 50,000 kwny unga huko.

No easy ride.
 
Chidi jiandae huyo jamaa akipata shida yeyote itabidi moto uelekezwe kwako na hautakuwa mdogo, wauzie wahuni wenzako maana revenge ni kwako tuu
 
Kwa US vitisho kama vya kina chidi ni kujitafutia kifo cha haraka sana, haijalishi kama unamtishia jirani au member wa crips gang, mnyamwezi atakufyatua ubongo bila hata kufikiria, kama humaanishi usimtishie mtu, adhabu ya kutomaliza ulichotishia inaweza kuwa kifo
 
Ukisikia wahuni ndo wale wala unga na wavuta bangi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…