Mradi wa Afya Shirikishi unachochea uwazi na uwajibikaji kwenye vituo vyetu vya afya

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Ikiwa Serikali pamoja na wadau wa Sekta binafsi wakiendelea na juhudi na mikakati tofauti ya kuboresha Sekta ya Afya Nchini ambayo utajwa kuzungukwa na changamoto mbalimbali, baadhi ya wananchi katika Kata ya Mkonze mkoani Dodoma wamefurahishwa na mradi wa Afya Shirikishi ambapo wamedai kuwa umewawezesha kufahamu wajibu wao katika ushiriki wa maswala ya afya pamoja na kuchochea uwazi na uwajibikaji katika kituo chao cha afya.

Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wa elimu iliyotokewa katika mradi wa #AfyaShirikishi unaotekelezwa na Asasi ya kiraia ya Wajibika,Shadrak Lucas ambaye Mwenyekiti wa Kamati ya Afya Kata ya Mkonze, amesema kuwa elimu hiyo imepelekea kushiriki katika masuala ya afya ikiwemo kituo cha afya kwenye Kata hiyo kuanza kuweka baadhi ya mambo wazi ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji.

" Ndugu zetu Wajibika wametusaidia pakubwa kabla hatujapata elimu waliotupatia tulikuwa hatujui vitu vingi lakini baada ya kupata semina na kufundishwa kwamba vitu gani sisi kama wanajamii tunatakiwa tuvijue kweli tumeona umuhimu, mfano siku za nyuma ulikuwa ukienda kwenye kituo cha afya unakuta uwazi wa mapato na matumizi haupo lakini kwa sasa tuliporudi tumekuta wameweka lakini siku za nyuma walikuwa haweki " amesema

Pia kwa upande wa mwakilishi wa wanufaika wa mafunzo hayo ambao yanatolewa na Wajibika, Christina Malogo, Mjumbe wa Kamati ya Afya Kata Mkonze amesema elimu wanayoipata imewaodolea hofu na kuchochea ushirikiano baina yao na wahudumu wa afya.

"Kwakweli tunashukuru Wajibika maana kipindi cha nyuma tulikuwa tunahisi tunanyanyaswa hatuwezi kuuliza chochote kwenye kituo cha afya, lakini sasa baada ya mafunzo hofu imeisha, kwanza tumkuwa marafiki na wale wahudumu wakina Mama wengi wanafurahi ilikuwa hata ukiona jambo ambalo sio rafiki huwezi kuuliza " amesema Mjumbe huyo

Aidha kwa upande wa watekelezaji wa mradi huo, John Mwilongo ambaye Mratibu wa Mradi wa Afya Shirikishi, kutoka Shirika la Wajibika amebainisha dhamira ya mradi huo.

"Mradi huu lengo la kuimarisha mifumo, utoaji na upokeaji huduma za afya kupitia ushirikishaji wa watoa huduma na wapokea huduma na kwasasa mradi huo unatekelezwa kwenye Kata nne mkoani Dodoma, Kata ya Mkonze, Matumbulu, Iumwa na Changombe kwa nyakati tofauti ikiwa tayari tumeanza na Mkonze"

Ameongeza kuwa "Tuliona kwanini kunakuwa na malalamiko ya wananchi kwamba nimeenda hospitali nimekuta huduma azilizishi, tukaona tuje na mradi huu ambao utajumuisha watoa huduma na wapokea huduma, hao wananchi wapate fursa ya kujifunza kwa karibu utoaji wa huduma kwenye vituo vyao ili wakienda pale wapunguze manunguniko ambayo yanaweza kuepukwa, lakini pia washiriki katika maendeleo ya kufanya maendeleo vituo vyao, kwa sababu watashiriki katika kupanga mipango ya kituo lakini pia watashiriki katika kutekeleza baadhi ya mambo pia watakuwa mabingwa (champion) katika kuelimisha wengine "ameeleza Jonh

Ikumbukwe Wajibika ni taasisi isiyo ya Kiserikali inayofanya kazi kuimiza mifumo ya uwajibikaji katika sekta ya afya, Elimu na Kilimo, lakini Mradi huo unaotekelezwa kwa sasa mkoani Dodoma kitengo cha afya.

Baadhi ya wadau utaja uwazi na uwajibikaji kuwa ni kiungo muhimu katika utawala bora.

20230523_131502.jpg

Nyakijoga
1684857859704.png

1684857905833.png
 
Back
Top Bottom