Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere, Rais Samia umetuheshimisha

Wacha porojo, weka mkataba mezani tuuone, tuamue kusuka au kunyoa, sio maneno meengi, mshaanza kutumika eehh, kwa manufaa ya matumbo yenu!?

We unasema mwendazake aligomea bila sababu za msingi, we umejuaje hakuwa na sababu ya msingi na mkataba hujauona!?

Uzalendo dhidi ya tumbo kazi..
 
umasikini wa akili ndio unatawala bongo nyingi za wanaomchukia magufuli.

angalia namna yao ya kujenga hoja ndipo utajua tatizo lilipo sio magufuli,bali wana chuki nayeye.
Hawa ni kuwaacha tu waendelee na ujinga wao
 
jambo moja ninalo jiuliza na kunishangaza ni moja tu nalo ni;
Bado Bandari ya DSM kuna matatizo, ufanisi wake bado hujafikia viwango vinavyo hitajika, bado kuna myanya ya upotevu wa mapato, sasa kwa nn tunataka kuharakisha bandari ya Bagamoyo wakati hiii tu ya DSM bado hatujaweza ku manage??!!
maoni yangu kwanza Serikali yetu na mamlka za Bandari ziboreshe badandari ya DSM, waongeze ufanisi wa vitendea kazi, wazibe myanya ya upotevu wa mapato ya serikali tukifanikisha na kudhibiti kikamilifu bandari ya DSM sasa tunaweza kwenda kifua mbele kwa Bandari ya Bagamoyo, vinginevyo tutazidi kutengeneza myanya ya wizi na ubadhirifu mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida kubwa ni pale tunapotaka kushindana na nchi jirani kwa kuyaacha nyuma maarifa yetu na kufanya kwa sifa bila hesabu za kuzidisha
 
Marehemu, nasita kutamka, lakini siamini kama alikuwa sawasawa. Kilichokuwa kinanishangaza ni namna alivyokuwa mwongo na kuendesha nchi kwa kuwahadaa watu ambao kwa kiasi kikubwa, walikuwa na uelewa mdogo.

Wengine aliwadanganya, akawajaza ujinga wa ajabu, mpaka leo wametopea kwenye ujinga waliojazwa na marehemu. Na wanaamini kuwa marehemu alikuwa kiongozi mzuri sana.

Katika marais wote tuliowahi kuwa nao, hakuna hata mmoja ambaye aliwahi kuwa mwongo kama marehemu.

Aliwadanganya watu kuhusu madini, aliwadanganya watu kuhusu gas, aliwadanganya watu kuhusu korosho, aliwadanganya watu kuhusu hali ya uchumi wetu, aliwadamganya watu kuhusu mradi wa Bagamoyo. Ilikuwa vigumu sana kwake kuhutubia hata mara moja, bila ya kuongea uwongo.

Siamini kabisa kama alikuwa sawasawa.
 
Mama yupo very much okay!Makosa akifanya tutamwambia.Kwa heshima nakuamkia!👍👍👍👍👍
 
VIP kuhusu kutoendeleza bandari zingine nchini
 
Yericko nyerere wewe ni nyumbu,ulikua na akili Kabla ya Slaa kuondoka.
Ulivyokubali kubiduliwa kwa gia za angani na ndo hapo unyumbu ulipoanzia
 
Pale Twiga ni upuuzi mtupu. Hakuna mabadiliko chanya. Ungejua kilichomo kwenye mkataba usingesifu chochote. Hakuna anayeweza kuutoa hadharani ule mkataba, kutokana na aibu. Magufuli was a good president for the fools.
 
Mataga ni kina nani? Utabaki na hilo jina mataga huku umasikini unakutafuna na wenzio wanapiga hela!

Usifikiri unapotetea ujinga unamkomoa Magufuli na familia yake hapana! Wanakomoka familia na ukoo wako huko vijijini
Aliyekwambia nimekuja hapa niwe tajiri ni nani?

Kwanza utajiri wenyewe ni mbaaayaaa kama nini maana kuupata lazima nijinyime, sasa naanzaje kujinyima na raha hizi zote za dunia?

Acha nile bata wewe endelea na mateso ya kusaka utajiri na ukoo wenu.
 
Alichokifanya Mbowe ni kuwageuza muwe mawakala sio kufikiria
 
Wewe ni mjinga!

Alidanganya watu kwamba nini?


Lowasa akiwa mgombea wa UKAWA wakati huo ikiwa bado haijabakwa alisema akiwa rais atahakikisha huo mradi anauvunja,

Magufuli alisema kasitisha huo mradi kwa kutoa dondoo za vipengele alivyosema ni mzigo kwa taifa!

Wewe jinga umekuja hapa kutetea unaweza kutuonesha ni kwa vipi alikuwa anadanganya?
 
Pale Twiga ni upuuzi mtupu. Hakuna mabadiliko chanya. Ungejua kilichomo kwenye mkataba usingesifu chochote. Hakuna anayeweza kuutoa hadharani ule mkataba, kutokana na aibu. Magufuli was a good president for the fools.
Kwanini usiweke hapa kilicbopo kwenye huo mkataba?
 
Ungewaacha wenye akili wajadili hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…