Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere, Rais Samia umetuheshimisha

Uko sahihi kwa 100%.
Tunataka tuone mkataba sisi wenyewe, tumechoka kupewa hadithi.
Kikwete alisema mkataba uko safi.
Magufuli akasema mkataba umejaa wizi.
Mama Samia anasema mkataba uko poa.
Nani mkweli?

Sasa ili kukata mzizi wa fitna, mkataba uwekwe wazi sote tuuone.
 
Unamuamini lowasa? Pole huyu aliyetudanganya atafia ccm ahami kamwe, Kisha akaenda chadema akaapa vilevile, Kisha akarudi Tena ccm
 
Hoja ipi?

Kuna hoja hapa zaidi ya kutetea ujinga mkiamini mnamkomoa mtu?
Nimkomoe nani? Nimkomoe marehemu? Kwani huo mradi ukiwa na manufaa au hasara, ataathirika marehemu? Yeye amemaliza safari yake, tuliobakia tuangalie kilicho chema kwaajili yetu na vizazi vijavyo.

Mimi siendeshwi na ushabiki au chuki kwa msingi wowote ule, naangalia kilichomo kwenye hoja.
 
Nchi hii ilishaingia mikataba mingi sana,kuna hata mmoja uliowahi kuona?.
 
Sasa wewe unatetea huo mradi ukisema waliotwambia una mapungufu waliongopa, je wewe unaweza kutuonesha manufaa yake katika utetezi wako?
 
Mbona mama anaongea bila ya kufokafoka?
 
Nami nikuulize, je una mkataba wa mradi wowote?
Unaweza kuiweka hapa tuisome?
Kama huna unafikiri ni kwanini mradi huu ni lazima mkataba wake ujulikane ilhal mikataba mingine hatuijui?
Tatizo hamjaamini kuwa huyu mwanamke wa shoka ndiye rais kwasasa
 
Dua za kuku bhana[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kuna point nimenasa. Tunatakiwa tujikite katika ujasusi wa kiuchumi.

Hivi kweli tumeshindwa kuzalisha mbegu za mafuta ya kupikia, mpaka tuagize nje na ardhi yote hii?

Hivi kweli tumeshindwa kuzalisha pamba na kutengeneza viwanda vya nguo kwa ajili ya hata soko la ndani , karibu wananchi 55m?

Inawezekana tunafeli katika ujasusi wa kiuchumi!
 
Nami nikuulize, je una mkataba wa mradi wowote?
Unaweza kuiweka hapa tuisome?
Kama huna unafikiri ni kwanini mradi huu ni lazima mkataba wake ujulikane ilhal mikataba mingine hatuijui?
Tatizo hamjaamini kuwa huyu mwanamke wa shoka ndiye rais kwasasa
Wale waliopigana kutokomeza utumwa, wangekuwa kama wewe mpaka leo utumwa ungekuwa ni ruksa..., sababu kama tulifanya hivyo huko nyuma kwanini tusiendelee kufanya hivyo, hivyo....
 
Sasa wewe unatetea huo mradi ukisema waliotwambia una mapungufu waliongopa, je wewe unaweza kutuonesha manufaa yake katika utetezi wako?
Miradi ya namna hiyo ipo kwenye mataifa mengi. Timu ya wataalam ilizunguka kwenye mataifa mengi kuangalia namna miradi ya namna hiyo jinsi inavyomilkiwa na inavyoendeshwa. Kwa kiasi kikubwa ilikuwa copy and paste. Mradi huu ulifanyiwa kazi na wataalam wengi kwa muda mrefu. Marehemu, sijui aliusoma kwa siku ngapi, akaufuta haraka haraka.

Alichokiona ni hiyo ya TRA kutofanya makusanyo ya moja kwa moja kwenye bandari. Na kingine ilikuwa ni umiliki wa miaka 99, akasema wamepewa wachina, jambo ambalo halikuwa kweli. Umiliki utakuwa kwa 3 entities - Tanzania, China na Oman.

Kwenye gas aliharibu kabisa, baadaye akadanganya kuwa gas wamepewa Wachina. Lakini wakati huo huo alimtuma Mwanasheria Mkuu kwenda kuwabembeleza wawekezaji warudi, wakakataa. Huku anawabembeleza, huku anasema gas imeuzwa. Sasa makampuni yaliyokuwa yanamiliki vitalu vya gas yataanza ujenzi wa LNG plant, uwekezaji wa dola bilioni 30, mwaka 2023. Kama gas iliuzwa China, hao wanakuja kuchimba gas gani?

Kwenye madini, Kabudi alifanya mabadiliko ya sheria ya madini, mabadiliko ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa very unprofessional. Kwenye mabadiliko yale, walisema in case of any dispute, makampuni yatalazimika kutumia mahakama za ndani. Lakini makubaliano na Barrick yanasema:

1) kama kuna dispute, pande mbili zitajitahidi kumaliza kwa njia ya maelewano.

2) wakati wa dispute, Serikali haitaruhusiwi kusimamisha uzalishaji

3) ukipita mwezi mmoja bila pande mbili kukubaliana, mahakama ya biashara ya Singapore itatarifiwa, nayo itatoa uamuzi, na uamuzi wake hautakatiwa rufaa popote

Masharti haya ni aheri hata yale yaliyokuwemo kwenye MDA wakati wa Kikwete. Hapa walionufaika ni Barrick.
 
Wale waliopigana kutokomeza utumwa, wangekuwa kama wewe mpaka leo utumwa ungekuwa ni ruksa..., sababu kama tunafanya hivyo huko nyuma kwanini tusiendelee kufanya hivyo, hivyo....
Hiyo sio dhamira yangu.
Ninachojaribu kueleza hapa ni kuwa usiri ndio jadi ya serikali ya ccm.
Kama walivyofanya usiri waliopita ndivyo mama atakavyofanya.
Hata ccm wanampigia kelele lkn wamesahau hata ndege hatujui bei zake.
 
Porojo tupu!

Ukiweka mkataba hapa hutakuwa na haja ya kuandika gazeti refu namna hii na uongo wa Magufuli utakuwa umejianika wazi.
 
Sasa wewe unatetea huo mradi ukisema waliotwambia una mapungufu waliongopa, je wewe unaweza kutuonesha manufaa yake katika utetezi wako?
Manufaa kwa Taifa na wananchi ni mengi, sawa kama ilivyo kwenye miradi yote mikubwa. Sina dababu ya kuorodhesha.

Kilicho dhahiri ni jinsi marehemu alivyodanganya kuwa eti TRA hawatakusanya chochote, na kuwa ardhi itamilikiwa na Wachina. Alitakiwa kuwaeleza wananchi ukweli, kama ilivyo kwenye mkataba, bila ya kupotosha.
 
Sasa kama marehemu unasema alidanganya kwa nini usiweke mkataba hapa tuone uongo wake?
 
Sasa usiwe unatuletea sisi huku stres zako
Stress nilikuwa nazo awamu ya 5 make iliharibu kwa kiasi miradi yangu. Ila awamu ya 6 hii ni biashara na bata tu kama awamu ya 4 vilee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…