mike2k
JF-Expert Member
- May 12, 2016
- 1,571
- 3,448
Katika miongo miwili iliyopita, tumeshuhudia uwekezaji mkubwa ukifanywa na Serikali ya Tanzania kwenye miundo mbinu ya usafiri na usafirishaji.
Ukiacha ujenzi wa barabara ulioongeza mtandao wa barabara nchini humo hadi kufikia zaidi ya kilometa 86,000, kuna miradi ya Reli ya SGR iliyowekezwa zaidi ya dola bilioni 1.2 ikitarajiwa kuunganisha nchi za Rwanda na Burundi, upo mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato, Dodoma, upanuzi wa bandari za Dar es salaam na Mtwara na ujenzi wa bandari mpya ya kisasa ya Bagamoyo.
Hapa kwenye bandari ya Bagamoyo, panaleta hisia mseto miongoni mwa watanzania kwa namna mradi huu, unavyotazamwa na kuchukuliwa na viongozi mbalimbali, na hisia mseto hizo zinaleta mitazamo kinzani inayozidi kuongeza 'ndimi' tofauti kwa wananchi wa kawaida.
Wapo wanaoona ni mradi mzuri ulio na manufaa kwa watanzania na wapo wanaoutazama kama mradi usiofaaa unaokuja kuinyonya Tanzania.
Nini kilichoko nyuma ya pazia na kwa nini ndimi mbili?
Mwezi Oktoba mwaka 2015, ujenzi wa mradi wa Bagamoyo chini ya Ukanda Maalumu wa Kiuchumi wa Bagamoyo (SEZ), ulizinduliwa rasmi na Rais wa awamu ya nne wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwenye uzinduzi huo alikuwepo Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi kutoka Usultani wa Oman Dkt. Ahmed Mohamed Al Furaisi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya China Merchants Group Dkt. Hu Jianhua kuashiria safari ya kuelekea kupata bandari itakayokuwa na uwezo karibu mara mbili ya Bandari ya Dar es Salaam ambayo kwa sasa ndio tegemeo na bandari kubwa nchini.
Kabla ya uzinduzi kulikuwa na majadiliano na mazungumzo ya muda mrefu kuhusu thamani ya mradi wenyewe, uwekezaji, ubia, hasara na faida zake, lakini ziara ya mwezi Machi mwaka 2013 ya Rais wa China Xi Jinping nchini Tanzania, na kusaini mikataba 16 na mwenyeji wake Rais Kikwete kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ilitoa picha ya namna utawala wa awamu ya nne ulivyoamini kuhusu mradi huu wa Bagamoyo na faida zake.
Hata Mwezi Julai mwaka huo, alipotembelea wakati huo Uwanja wa Sabasaba kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa (DITF), Rais Kikwete alitangaza neema kwa wakazi wa Bagamoyo ambayo wangeathirika na ujenzi huo, ikiwemo kubomolewa makazi yao.
'hakikisha mnawasiliana na Bandari jinsi gani ya kuwalipa fidia wakazi wa bagamoyo mtakaowahamisha kwa kuwajengea nyumba sehemu nyingine ili wakazi hao wasiyumbe kiuchumi', alinukuliwa Rais Kikwete alipokuwa akimpa maagaizo Mkurugenzi wa wakati huo wa Mamlaka ya Ukanda wa Uwekezaji (EPZA), Dk. Adelhem Meru.
Lakini kabla ya ujenzi kufika popote Mwezi Mei, 2019 Serikali ikalitaarifu bunge la Tanzania kwamba Mradi mkubwa wa Ukanda Maalumu wa Kiuchumi wa Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) umefutwa na hautafanyika tena.
Juni 7, 2019 Rais wa awamu ya Tano, John Pombe Magufuli aliyeingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2015 kuchukua nafasi ya Rais Kikwete aliueleza umma kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kwanini ameamua kufanyauamuzi huo? na alinukuliwa akisema "kwenye mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo kulikuwa na vipengele vya hovyo".
vCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Rais Magufuli
Kabla watanzania hawajasahau kauli hiyo ambayo waliiamini kwa sababu imetoka kwa kiongozi wao, miaka miwili baadaye (Juni 26, 2021), Rais wa awamu ya 6, Samia Suluhu ambaye alikuwa makamu wa Rais wakati wa utawala wa Rais Magufuli, kwenye mkutano mwingine wa baraza la taifa la biashara akaja na kauli ingine ya kufufuliwa kwa ujenzi wa bandari hiyo.
'tumeanza mazungumzo (na mwekezaji) ya kufufua mradi wote ule wa Bagamoyo ili nao tuufungue twende nao kwa faida ya taifa letu na kwa faida ya wawekezaji pia', alisema Rais Samia kwa ufupi.
Huenda kauli hii haimaanishi kutoyaona masharti ya hovyo aliyoyaona mtangulizi wake John Pombe Magufuli, lakini inatoa picha ya namna mradi huu unavyopaswa kutazamwa mara mbili mbili, ili kujenga Imani kwa watu kutokana na kauli za mamlaka.
Kauli hii ilikuwa ya matumaini kwa waliokuwa wanapigia chapuo ujenzi wa bandari hii, ikionekana kuwa na mtazamo sawa ama unaokaribiana na ule wa utawala wa awamu ya nne kuhusu ujenzi wa Bagamoyo.
Lakini kwa wale walio ishika vyema kauli ya magufuli kuhusu "masharti ya hovyo" kurejeshwa kwa mradi huu ni mwiba jichoni.
'Mradi huu mkubwa wa uwekezaji ambao thamani yake ni zaidi ya Bajeti ya Maendeleo ya Wizara nzima ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa miaka minne (TZS 18 Trilioni) haupaswi kufutwa tu bila mjadala wa kina', ilikuwa kauli ya kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT- Wazalendo kuonyesha kutofurahishwa na kauli ya kufutwa kwa mradi huo.
Sasa mijadala imeibuka hasa, na maswali lukuki yakiulizwa, likiwemo la kwanini kuna kauli 'ndimi' mbili kuhusu mradi huu?
Hakuna anayeweza kuwa na jibu thabiti la kauli hizi, lakini inasalia kusemwa faida za mradi huu, haziwezi kuepukwa na hasara kadhaa zinazoonekana kwenye picha nzima ya mradi.
Kwanini ujenzi wa bandari hii unapigiwa chapuo?
Unaweza kutaja faida zake ndio msingi wa mradi huu kupigiwa chapuo na wanaoutaka.
Wengi wakisikia ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, wanaishia kwenye kufikiria kuhusu bandari yenyewe tu, lakini kwa mujibu wa mkataba wa mradi huu wa Bagamoyo SEZ, kunatarajiwa kujengwa pia viwanda karibu 880, awamu ya kwanza ya ujenzi wa viwanda hivi vitajengwa viwanda 190.