SoC04 Mradi wa BBT kwa Vijana ufanyike kila wilaya na uunganishwe na VETA Pamoja na 10% ya Halmashauri iliyoboreshwa

SoC04 Mradi wa BBT kwa Vijana ufanyike kila wilaya na uunganishwe na VETA Pamoja na 10% ya Halmashauri iliyoboreshwa

Tanzania Tuitakayo competition threads

ngatungas

Member
Joined
Sep 16, 2021
Posts
5
Reaction score
13
Ni wazi kwamba Ajira kwa vijana imekuwa ni kilio kwa kila Familia hapa nchini.
Na hata kuwa Agenda/Fursa kwa wanasiasa pia.
Ila mwiba wa hicho kilio kinapaswa pia kianzie na sera madhubuti zilizoboreshwa zinazolenga kutatua changamoto hii.

BBT KWA KILA WILAYA
~• mradi huu wa Building Better Tomorrow ni mradi mzuri wa kimkakati wa kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri na kutatua changamoto za kimaisha.

~• Tatizo ni kwamba mradi huu vijana wanapelekwa kambini na kujifunza shughuli mbalimbali za kilimo na ufugaji pasipo kuzingatia sehemu watokayo.

~• ilipaswa kuwe na kambi katika kila wilaya husika,Maana kila wilaya ina vitega uchumi vyake na aina kadhaa ya mazao na ufugaji unaofaa kulingana na mazingira husika. Na ingebeba vijana wengi maana wangeweza kwenda asubuhi na kurudi makwao jioni.

BBT & VETA
• katika Miradi hiyo husika kwa kila wilaya,huendana na utumiaji wa nyenzo sahihi ili kuleta Matokeo bora ya mradi. MFano, Zana za kisasa za uvunaji mazao ya nyuki, ukamuaji ng’ombe maziwa, pamoja na uchakataji wa mazao hayo katika kuyaongezea thamani.
Pia utumiaji wa vifaa kama Drones, Drip systems katika shughuli za kilimo na umwagiliaji.
Yote haya VETA inaweza fundisha vijana hawa utumiaji sahihi wa vifaa hivyo.
• Na Vijana hao pia wanaweza fundishwa ujasiriamali jumuishi wa kujenga viwanda vidogo vya uchakataji mazao ya kilimo,usindikaji na upakiaji. Hivyo kutoa Ajira kwa kundi jipya la vijana na serikali kupata mapato zaidi.
• Hizi VETA zikiwa kimkakati zaidi zinaweza bobea katika nyanja husika kwa kila wilaya, na hata kuimarisha teknolojia hitajika kwa kuwa zitakuwa zimejikita kwa uzoefu kuzalisha wataalamu wa kutumia/kutengeneza vifaa husika kwa kila wilaya fulani.

BBT, VETA & 10% YA HALMASHAURI

-> Miradi yote hiyo jumuishi ya BBT na VETA haitaweza fanikiwa bila mitaji thabiti.

-> Na sote tunajua jinsi gani ilivyo ngumu kwa biashara mpya/ mradi mpya inayochipukia yenye mawazo mazuri ilivyo ngumu kupata Mikopo kwenye taasisi husika bila ya kupata mtu wa kukushika mkono.
Japo BBT wamejinasua kwa kuwapa mashamba,pembejeo na Mifugo kama kianzio, fungu hilo la halmshauri pia linaweza wapa nguvu kwa kuanzisha viwanda vidogo vya uchakataji, ufungashaji na uongezaji thamani.

-> Pia katika hiyo 10% ya Halmshauri ilipaswa iboreshwe kwa kuweza kutoa mikopo hata kwa mtu mmoja mmoja.
kwa maana sote tunajua inaumiza pale mnapopewa mkopo kwa kikundi na baadhi yenu wakakengeuka na kusababisha mliobaki muingie gharama za kuhakikisha rejesho linakamilika.

Kadhalika kuna vijana ambao hua na wazo la kipekee linaloweza leta tija kwa wilaya na hata kuzalisha ajira kwa wengine.

Halmshauri zinaweza pitia MAANDIKO ya wahitimu wa Mafunzo hayo na kucheki miradi husika pendekezwa na hata kuwapa mikopo kwa awamu na kwa kiwango sahihi.

Kwakuwa wengi hawana Asset ziwe kama Dhamana kwenye BANKS & FINANCIAL INSTITUTIONS.

-> hivyo tutaongeza uzalishaji kwa kila wilaya husika na kuongeza upatikanaji wa Ajira na ujuzi na hata kuweza kuzalisha PRODUCTIONS ZONES za Mazao husika yaliyoongezwa thamani zaidi.

-> kama tunavyoona kwa wenzetu CHINA kwa kila jimbo kubobea kwa uzalishaji wa bidhaa fulani.
Na kuwepo kwa MARKET ZONES ambazo zinahusika na Mauzo tu ya bidhaa hizo.

-> Raw materials tunazo, Ardhi tunayo ya kutosha na Nguvu kazi vijana tunayo. Hivyo tukijipanga katika sera zetu vilivyo TUNAWEZA.

KWA HITIMISHO
BBT, VETA na halmshauri ni taasisi za serikali ambazo zinaweza fanya kazi kwa pamoja kuwezesha vijana.
  • Ambapo pia wanaweza waunganisha na SIDO kuwapa mashine na vifaa husika ili kufanikisha miradi yao.
  • Halmshauri pamoja na wenyeviti wa kila mitaa ambapo wanafahamu vijana hao ni rahisi kuwasimamia pale wanapotekeleza miradi hiyo na kuhakikisha matumizi sahihi ya rasilimali wanazopatiwa.
  • Itapunguza wimbi la vijana kuhamia miji mikubwa , hivyo kukuza ustawi wa wilaya husika na kuchagiza maendeleo katika kila kona ya nchi. Na kuwepo kwa majiji mengi.

AHSANTE!
 
Upvote 5
Back
Top Bottom