Mradi wa golf Songea manispaa umekwama wapi?

Mradi wa golf Songea manispaa umekwama wapi?

kindigiwa

Member
Joined
Apr 5, 2020
Posts
85
Reaction score
133
Habari Wana jamvi,mwaka 2021 halmashauri ya Manispaa ya Songea ilikwenda kata ya Subira iliyopo Manispaa ya Songea na kuhitaji ardhi zaidi ya ekari 300 kwa maelezo kuwa wana jenga mradi mkubwa wa mchezo wa golf.

Mradi huo ungehusisha ujenzi wa five star hotels, shopping mall na vivutio vingine.

Mbunge wa Jimbo la Songea mjini ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Maliasili na utalii alieleza kuwa miongoni mwa faida zitakazo patikana kwa Wana songea na Tanzania kwa ujumla ni kuwa mradi huo uta chochea utalii katika mkoa wa Ruvuma na mikoa jirani ukiachilia mbali ajira za Moja kwa Moja na za muda.

Zoezi la uthamini ardhi na Mali zilizomo katika eneo hilo linalo twaliwa kwa mujibu wa Sheria lilifanyika na hadi Sasa hakuna malipo yaliyo fanyika na hakuna lolote linalofahamika ikiwa ni kama mpango bado upo au ulikwisha kufa!

Wakati wa zoezi la uthamini wamiliki walielezwa (na watendaji wa uthamini)kuwa tayari pesa za kulipa fidia zipo na kwamba mradi huo ulitakiwa kuanza kutekelezwa mara Moja!hadi Sasa wamiliki wa ardhi Ile inayo twaliwa kwa mujibu wa Sheria wapo njia panda hawajui Cha kufanya miongoni mwao walihitaji kuendeleza maeneo Yao kwa namna mbali mbali ikiwemo kilimo Cha mazao ya muda mrefu na mfupi,ujenzi wa makazi nk.

Miongoni mwao wamo watu ambao walikwisha andaa tofari kwaajili ya ujenzi wa makazi Yao ili wahepukane na hadha za kupanga lakini bado wamo katika mikiki mikiki ya kupanga kwa kuwa wana shindwa kujenga nyumba zao katika maeneo Yao ambayo yana twaliwa kwa mujibu wa Sheria.

Ikumbukwe kuwa wakati wa uthamini huu wamiliki wa ardhi walilalamika kuwa fidia ya shilingi laki Saba kwa ekari Moja ya ardhi ni ndogo walionekana Wana zuia maendeleo ya Wana songea na Tanzania kwa kutaka fidia kubwa!
Hadi Sasa wamiliki hao Wana jiuliza kati ya mamlaka na wao ni nani anayekwamisha maendeleo?

Wamiliki wanaomba mamlaka za juu ziwasaidie ili ama walipwe fidia na wao waende kutafuta ardhi mahali kwengine maisha ya endelee au wapewe ruhusa ya kufanya shughuli zao katika eneo lile,au waelezwe chochote kuhusu mradi huu kwani ukimya wa halmashauri ya Manispaa unawapa wakati mgumu!
 
Nenda hapo ofisi ya mbungen nssf gorofa ya tatu watakupa majibu au ofisi ya mkurugenzi manispaa
 
Back
Top Bottom