Mradi wa Kilimo cha Pamba

Mradi wa Kilimo cha Pamba

Mfugaji123

New Member
Joined
Apr 3, 2020
Posts
4
Reaction score
42
Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazozalisha pamba kwa wingi. Kulinga na na taarifa ya Bodi ya pamba, Tanzania huzalisha wastani wa tani 220,000 za pambambegu kwa mwaka. Na huwakilisha asilimia 10 ya mapato ya nchi yaani GDP. Taarifa za sasa zinaonesha pamba ni chanzo cha kipato kwa kaya takribani laki tano yaani sawa na watu wapatao milioni 2. Pamba ya Tanzania inajulikana kwa ubora wake katika soko la dunia, kwa sababu hutokana na aina pamba ndefu ya wastani ambayo ina bei kubwa katika soko la dunia. Ubora huu wa pamba ya Tanzania huifanya iweze kushindaniwa katika soko la kimataifa katika mabara ya Asia, Ulaya na baadhi ya nchi za Africa
Soko la dunia linachochewa zaidi na kuongeza kwa matumizi ya pamba katika viwanda mbalimbali ikiwemo kutengneza nguo, vifaa vya viwandani , nyiumbani na hospitali. Pia mafuta ya pamba hutumika katika kupikia, kutengeza sabuni na vipodozi. Pamaba sasa inaitwa dhahabunyeupe na serikali kupitia bodi ya pamba inapigia chapua zao hili kwa kuhamasisha wakulima kulima zao hili. Kwa sasa bodi huto mbegu, viuatilifu na mabomba ya kunyunyiza dawa kwa mkopo ambapo wakulima hulipa mkopo huo baada ya kuuza pamba. Hata hivyo, ukweli ni kama serikali hutoa pembejeo hizo kama ruzuku kwa sababu hakuna mkulima ambaye hudaiwa baada ya kuuza pamba

RIPOTI YA UPEMBUZI YAKINIFU YA MRADI WA KILIMO CHA PAMBA
Ripoti ni ya mradi wa kilimo cha pamba katika ekari 1000 . Upembeuzi umechambua maeneo yanayofaa kulima pamba, upatikanaji wa ardhi/ mashamba, mbegu na pembejeo zingine kama viuatilifu na mbolea. Ripoti pia imechambua mwenendo wa masoko, bei za pamba na faida za kilimo cha pamba sasa na siku za hivi karibuni. Ripoti hii pia imefanya uchambuzi wa kifedha gharama za kulima ekari 1000 pamoja na mapato na faida tegemewa. Ripoti inaweza kutumiwa na makampuni au watu binafsi kuamua kuwekeza katika kilimo hiki
FUNGUA LINK HII KUPATA RIPOTI KAMILI HAPA

FUNGUA LINK HII KUPATA RIPOTI HII
 
Back
Top Bottom