Wanajamii narejea tena katika mtandao nikiwa na mada ya Mradi wa Magari yaendayo Kasi Jijini. katika mada hii nataka wanajamii tufanye utafiti wa kujua mara mradi huu utakapokamilika wazawa tutawezaje kununua hisa ili tumiliki mradi huu na tuweze kujipatia kipato cha kujikimu katika mchakato wa maisha. Ni muhimu sana kama kweli Serikali yetu itakuwa na nia njema kwa wananchi wake kuwawezesha kumiliki hisa za Kampuni itakayokuwa inaendesha huduma za usafiri jijini. Siku za leo mpango mzuri wa kufanya biashara ni kuingia ubia.
Nina hakika mkaaji wa Bongo anajua umuhimu wa usafiri, tabu iliyopo sasa ya usafiri na hitaji kubwa la usafiri jijini. Hivyo ukiwekeza katika biashara hii hakuna kupata hasara hilo nina hakika nao tena kwa mtazamo usio wa kisayansi kabisa.
Ombi kwa wanajamii mwenye dondoo za jinsi itakavyokuwa atujuze na kama hakuna kinachoeleweka mimi kwa ufahamu wangi mdogo hii ni fursa kubwa sana tafadhali tuungane kuwataka hawa wakubwa wetu fursa hii waitoe kwa wananchi. Maana yangu Elimu itolewe kwa umma na kuwataka hao wawekezaji kutoa fursa ya wananchi wanaohitaji kununua hisa wanunue.
Zilikuwepo fursa kama UTT yaani Umoja Fund na zingine wanachi hawakuwa na taarifa za kutosha juu ya ununuzi wa hisa hivyo wengi hawakuweza kununua na tena wanashangaa neno lenyewe HISA ni nini?.
Kwa habari ya Mradi huu mimi bila hiyana nasimama kidete kuwakumbusha na kuwaamsha waliolala kwa mbiu ya "Chonde chonde wanajamii fursa hii ni haki yetu tuichamkie". Naomba wadau mbali mbali wenye ufahamu na mambo haya wanasiasa na wote wenye mapenzi mema na watanzania wenzao juhudi za makusudi zifanyike kuhakikisha wananchi wanapata umiliki katika Kampuni itakuyofanya shughuli hii ya kwasafirisha wakazi wa Dar.
Mimi nitakuwa mmoja kati ya watu wa mwanzo kununua hisa kama fursa hiyo itakuwepo pia niko mbele kama nitajulishwa taarifa muhimu zihusuzo jinsi ya kuhakikisha wananchi wanapata fursa hii. Naomba tena mwanajamii yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia tadhali rusha katika mtando ama Private message au email yangu kazimosco@gmail.com.
Naomba tuwe wazalendo tujenge mshikamano ili tusonge mbele kiuchumi. Uwanja na uwacha kwenu.