KERO Mradi wa maji Kata ya Ruzinga haujakamilika tokea 2012, maji hutoka pale kunapokuwa na ziara ya kiongozi

KERO Mradi wa maji Kata ya Ruzinga haujakamilika tokea 2012, maji hutoka pale kunapokuwa na ziara ya kiongozi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kata ya Ruzinga wilaya ya Missenyi Mkoa wa Kagera kuna mradi wa maji haujawahi kamilika toka mwaka 2012 hadi watu washachoka kulalamika maana ukijaribu kufuatilia taarifa zinasema mradi ushakamilika ila kiuhalisia maji yanayotoka hayatoshi.

Mara nyingi huwa yanatoka tu pale kama kuna kiongozi anakuja na akiondoka mradi unakwama tena.

Natumia jukwaa hili kupaza sauti Serikali ituangalie kwa jicho la tatu maana tunajua hawana taarifa kama huu mradi haukukamilika.
 
Miradi mingi ya maji ni ovyo kabisa na hakuna uwajibikaji. Akashaija butege kateneka sho.
 
Back
Top Bottom