Mradi wa Maji Taka unaofanyika Sinza D (Madukani) una kasoro kadhaa zinaweza kuwa na athari, uangaliwe upya

Mradi wa Maji Taka unaofanyika Sinza D (Madukani) una kasoro kadhaa zinaweza kuwa na athari, uangaliwe upya

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Sinza D (Mtaa wa Sinza Madukani) kuna mradi wa uchakataji wa maji taka unaofanyika chini ya usimamizi wa karibu wa Diwani wetu ukifadhiliwa na Benki ya Dunia na kuratibiwa na DAWASCO, ambapo unatarajiwa kukusanya maji taka toka kwenye nyumba 500.

Maji taka hayo yatapitishwa kwenye bomba ndogo kuelekea kwenye Septic Tank ambalo litajengwa pembeni ya Mto Ng’ombe.

Inayoonekana ni kama mradi unaendeshwa bila kuzingatia taratibu au unaendeshwa Kisiasa, sababu ya kusema hivyo ni kwamba kwanza hakuna ushirikishwaji wa karibu kati ya wahusika wa mradi na Wananchi.
WhatsApp Image 2025-02-14 at 11.36.50_a989cd14.jpg

Hizo za blue ni bomba za kupitisha maji taka (kinyesi) toka kwenye nyumba 500, na hilo bomba la kijani ni bomba kubwa la maji safi, pamoja na bomba hizo ndogondogo zinazoelekea katika nyumba za Watu, ukaribu wa hivi ni unaweza kuwa hatarishi ikitokea kuna mwingiliano.
WhatsApp Image 2025-02-14 at 11.37.24_cb5d4068.jpg

WhatsApp Image 2025-02-14 at 11.37.25_c097a9ad.jpg

Mradi umeanza bila ya Watu afya na mazingira kuja kutoa elimu juu ya athari za mradi, bomba za maji taka zinazotandazwa hazizidi ukubwa wa Inch 6, kina kwenda chini ni mita moja, kwa urefu huo ni hatari kwa kuwa ni rahisi kufumuka.

Mtambo wa uchakataji wa maji taka unatarajiwa kuwekwa pembeni ya nyumba ya mtu na karibu kabisa na Mto Ng’ombe.

Tulihoji baada ya kuchakata Maji taka watafanyaje, wakasema yatakuwa safi lakini hayatafaa kutumika katika umwagiliaji wa mazao kama mbogamboga, lakini watayamwagia katika Mto Ng’ombe.

Sote tunajua kuwa Mto huo kwa mbele kuna watu ambao wanayatumia hayo maji kumwagilia mbogamboga, unadhani nini kitatokea?
WhatsApp Image 2025-02-14 at 11.34.44_6e82df4a.jpg

Siku wanaandaa sehemu ya Bwawa walichoma moto ambao moshi wake ulikuwa mwingi na ulidumu siku nzima hali iliyokuwa kero kubwa kwetu na kutuathiri kiafya.
 
Back
Top Bottom