salaam wana jf!
Kuna mradi mkubwa wa kujenga nyumba za kuuza unaoratibiwa na pspf, ppf nadhani na nssf uliopo eneo liitwalo buyuni - chanika jijini dar es salaam. Ninamiliki kiwanja eneo hilo pia na hati ninayo. Nimefika eneo hilo leo nikakuta nimezungukwa na nyumba zilizokwisha anza kujengwa na hayo mashirika. Niliowakuta eneo hilo kwa leo wakaniambia huwa wanajenga kiwanja chochote kilichowazi/hakijaendelezwa.
Kwa mwenye kufahamu juu ya hili naomba kufahamishwa.
Nawasilisha
Du umenitisha!!! maana tuna kiwanja na sie huko. Sidhani kama wana mamlaka ya kufanya hivyo bila hata kututaarifu. Any way ntaenda na mimi kesho huko.
hizo nyumba ni nzuri?
Utaratibu wa kuzinunua ukoje?
Bei zake zikoje?
Na lini wataanza kuuza?
Asante!
Wana viwanja vyao wala hawagusi kiwanja cha mtu...subiria zikiisha ukaombe kununua zipo kama 800 hivi!
Kaa utulie na kiwanja chako!!