Mabadilishano ya kirafiki kati ya China nan chi za Afrika, amayo yamedumu kwa muda mrefu, yameongezeka zaidi katika miaka ya karibuni, na kuhusisha Nyanja mbalimbali ikiwemo siasa, uchumi na utamaduni. Mradi wa televisheni za setilaiti kwa vijiji 10,000 barani Afrika unaotekelezwa na China umesaidia kutangaza kugha za asili katika maeneo ya vijijini barani Afrika kupitia tamthilia zinazowekwa sauti kwa lugha za maeneo husika.
Katika kijiji cha Bunono karibu na mji wa Entebbe nchini Uganda, wanakijiji wanajadiliana kwa furaha kuhusu Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2024, na kukumbuka jinsi, zamani, walivyokuwa wakiweza kuangalia mechi kwa matangazo ya lugha ya kiingereza tu, lakini sasa, wanaweza kusikiliza matangazo hayo kwa lugha yao ya asili, Luganda.
Kampuni ya StarTimes ya mjini Beijing, imewezesha hatua hiyo kupitia mradi uliopendekezwa na China wa “Kupatikana kwa Televisheni za Setilaiti kwa vijiji 10,000 vya Afrika,” unaolenga kuunganisha vijiji 10,000 barani Afrika na vipindi vya televisheni kupitia satelaiti.
Mpaka kufikia mwezi Desemba, 2023, mradi huu ulishuhudia kukamilika kwa mafanikio kazi ya ujenzi katika nchi 20 za Afrika, kujumuisha vijiji 9,512 na kunufaisha moja kwa moja zaidi ya kaya 190,000. Chini ya mradi huo, kila kijiji kilipokea seti mbili za televisheni zinazotumia projekta za umeme wa jua na televisheni moja iliyo na mfumo kamili wa kidijitali kwa ajioli ya maeneo ya umma bila malipo, kama ilivyothibitishwa na mkandarasi ambaye ni kampuni ya StarTimes.
Wakati wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2024 yaliyofanyika kuanzia Januari 13 hadi Februari 11, matawi ya kampuni ya StarTimes katika nchi za Uganda, Rwanda, Nigeria, na Tanzania yaliajiri wataalamu wa michezo ili kutangaza mechi hizo kwa lugha sita za huko, hatua iliyopokelewa vizuri na watu wa huko. Kampuni ya StarTimes inalenga kuboresha lugha mbalimbali katika vipindi vyake vya kidijitali kupitia setilaiti kupitia mfumo wa lugha wa Akili Bandia (AI), na kusaidia kudumisha lugha za asili katika maeneo ya ndani zaidi barani Afrika.
Wakati televisheni za kidijitali kutoka Magharibi zinalenga zaidi katika soko la matajiri barani Afrika, kampuni hii ya China inajikita zaidi katika soko kubwa la vijijini katika bara hilo, na kuwa mchezaji muhimu katika kuondoa kikwazo cha ukiritimba wa taarifa na utamaduni, na kusaidia Waafrika wengi zaidi kuingia katika dunia pana na nyumbufu zaidi kupitia lugha zao za asili.
Ili kuwezesha watu wengi katika maeneo ya vijijini barani Afrika kutazama vipindi vya televisheni na michezo ya kuigiza ya Kichina ambayo wanaweza kuelewa hakuwezi kutenganishwa na wataalamu wa kutia sauti. Hata hivyo, ilikuwa ni vigumu katika siku za mwanzo kupata wataalamu wa kutoka kutoka Afrika wanaoweza kutia sauti kwa lugha za asili za Afrika hapa nchini China.
Tangu mwaka 2016, StarTimes imefanya mshindano 23 ya kutafuta wataalamu wa kutia sauti katika tamthilia na filamu za China katika nchi tano, Tanzania, Nigeria, Cote d’Ivoire, Afrika Kusini na Msumbiji, na hivyo kutatua tatizo la ukosefu wa wataalamu wa kutia sauti. Watu walioonyesha ustadi mkubwa walikaribishwa Beijing kwa mafunzo na kufanya kazi, na hivyo kufuata njia ya ajira itakayowawezesha kuwa wataalamu katika sekta ya habari.
Shogotera, mmoja wa wataalamu hao kutokea Mwanza, Tanzania, kwa sasa ni daraja la mabadilishano ya kitamaduni kati ya China na Afrika. Anapenda kusimulia hadithi za China na kuondoa uelewa mbaya kuhusu China. Kama msomi wa historia, anaamini kuwa njia ya maendeleo ya China ni ya amani zaidi kuliko nchi nyingine. Anasema katika maskani yake, njia nyingi za reli, vituo vya kuzalisha umeme, na miundombinu mingine vimejengwa na kampuni za China. Anaona kuwa, juhudi hizo zinamfanya aipende zaidi China na kumfanya kutaka kuelewa kwa undani zaidi China halisi.