Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
"Nitoe taarifa kwamba kuna mradi wa makumbusho ya Marais, mradi huu ni mradi no 5221 eneo liko Mtumba na tumetenga bilioni 34 kwa ajili ya mradi huu na mwaka huu tumeanza kutenga bajeti ndogo kama bilioni 1 na eneo lile lina ukubwa wa Ekari 50," - Rais @SuluhuSamia. #UzinduziKitabuChaSokoine
Mtazamo na maoni yangu. Je, kama Taifa tunauhitaji huo mradi kwasasa!? Jibu ni HAPANA maana tayari tuna mzigo mkubwa kuhudumia wenza wao kwasasa ambao wote bado wako hai:
Kuchoma billion 34 kwenye mradi kama huu sidhani kama mamlaka zimeshauriana vema. Afya ya Jamii ni jambo la muhimu na la msingi sana. Kama tulithubutu kufuta bima ya mtoto yenye thamani ya bilion 20 kwa mwaka tunapata wapi uthubutu wa kuleta mradi wa nakumbusho ya maraisi wa billion 34?
Tuna mahitaji mengi ya lazima kama taifa na haya ndio lazima yapewe kipaumbele .. Elimu, maji safi, lishe bora, vifaa tiba.. Wataalam wa afya,wataalam wa kilimo mikopo nknk.. Huko kunahitaji kupewa kipaumbele hasa kwakuwa kunayagusa maisha ya taifa hili moja kwa moja kila siku kila saa na kila dakika
Makumbusho ya maraisi ukiachana na historia Pia ni jambo la kifahari zaidi. Wanaofanya mambo ya kifahari tayari wana ziada!
Pia, soma: Serikali yatenga Shilingi Bilioni 34 kujenga Makumbusho ya Marais Dodoma

- Matibabu yao
- Mishahara
- Nyumba mpya
- Magari mapya kila baada ya muda
- Matumizi yao ya kila siku nk
Kuchoma billion 34 kwenye mradi kama huu sidhani kama mamlaka zimeshauriana vema. Afya ya Jamii ni jambo la muhimu na la msingi sana. Kama tulithubutu kufuta bima ya mtoto yenye thamani ya bilion 20 kwa mwaka tunapata wapi uthubutu wa kuleta mradi wa nakumbusho ya maraisi wa billion 34?
Tuna mahitaji mengi ya lazima kama taifa na haya ndio lazima yapewe kipaumbele .. Elimu, maji safi, lishe bora, vifaa tiba.. Wataalam wa afya,wataalam wa kilimo mikopo nknk.. Huko kunahitaji kupewa kipaumbele hasa kwakuwa kunayagusa maisha ya taifa hili moja kwa moja kila siku kila saa na kila dakika
Makumbusho ya maraisi ukiachana na historia Pia ni jambo la kifahari zaidi. Wanaofanya mambo ya kifahari tayari wana ziada!
- Je, sisi kama taifa tunayo hiyo ziada!?
- Vipaumbele vyetu ni vipi kwenye mambo ya msingi?
- Vipaumbele vyetu ni vipi kwenye mambo ya lazima?
- Vipaumbele vyetu ni vipi kwenye mambo muhimu?