Hivi ni Mungwana yupi atawapereka mafisadi segerea. Bado mna tumaini kuwa iko siku huyo mungwana wenu atawapereka. Pole sana Tanzania.
Tanzania aksante kwa kutupa pole watanzania wenzako ni kweli tunaistahili.
Umeuliza nani atawapeleka mafisadi segerea I tell you tukisubiri wapelekwe basi tutasubiri milele na tutakufa bila kelele. Tusisubiri wapelekwe TUWAPELEKE SISI WENYEWE wananchi walia juani.
Umesikia F.M akisema kuwa nguvu ya ukabila sijui umkoa imetumika ni wazi kuwa ni sisi wenyewe ndio wa kulaumiwa na ni sisi wenyewe tunaokubali kuchezewa ngoma ya unyago au kumtoa mwali juu ya vichwa vyetu. SSIS kama wananchi tunaouwezo wa kubadili haya yote only if tutabadilika na kujua umuhimu wetu katika kuijenga Tanzania tuitakayo.
Kama wananchi wenyewe wa Kilimanjaro wameamua kumchagua fisadi kwa sababu zao binafi ni wazi kuwa something is wrong somewhere! Na waelewe kuwa katu si Rais, wala waziri mkuu atakayesimama na kutetea haki zao ni WAO WENYEWE.
Hivi ingekuwaje kama wao waKilimanjaro wangeshikamana na kupiga kwa Mramba kusimamishwa kama mgombea wa nafasi hiyo?
- Itakuwaje pale waTanzania tutakapokuwa na ujasiri wa kusimama barabarani na kuprotest kwa mafisadi kuwa huru kwa dhamana(pamoja na kuwa dhamana ni haki yao?)
- Itakuwaje kama waTanzania tutashikamana na kusema SASA BASI TUMECHOKA kuchezewa na uongozi huu unaolea mafisadi na kila aina ya UOZO?
- Itakuwaje tukisimamisha shughuli zetu japo kwa wiki moja na kutanda mabarabarani na mabango yetu tukidai HAKI zetu?
UWEZO U JUU YETU NI KUUVAA TU UJASIRI.