Nairobifly
Member
- May 3, 2012
- 75
- 26
Ni mratibu wa tasaf wilaya ya Ngorongoro. Wakiwa ktk harakati za kuanza safari toka Karatu kwenda Ngorongoro dereva alimwomba bosi wake wapitie gereji kabla ya kuanza sfr ili kurekebisha matatizo madogo kwenye gari. Baada ya kufika gereji dereva alikabidhi gari na ufunguo kwa fundi, bosi wake akiwa ndani na yeye kutoka kidogo. Marekebisho ya gari hayakuwa makubwa hivyo fundi alimaliza kazi yake mapema. Bosi alikaa takiribani nusu saa akiwa anamsubiri dereva wake bila mafanikio na pia alikuwa hapatikani kwenye simu. Baada ya kuona hivyo akachukua uamuzi wa kuondoka na kumuacha dereva yule. Kilichofuata baada bosi kuondoka ni kwamba dereva ilibidi atafute usafiri private wa kwenda Ngorongoro. Taarifa zinilizopata hivi punde ni kwamba dereva yule amemburuza bosi wake polisi kwa kitendo cha kuchua gari bila ridhaa yake. Je,wandugu kati ya wawili hawa yupi mwenye makosa? Source:nimeshuhudia mwenyewe