Mratibu wa kampeni za Freeman Mbowe ametoa kauli kali akiwataka wale wanaomtuhumu Mwenyekiti huyo wa CHADEMA kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha mara moja, akisisitiza kuwa ni kumkosea heshima kiongozi huyo.
Akizungumza na Jambo TV, mratibu huyo ameeleza kuwa Mbowe ameonyesha uongozi wa kipekee na kujitolea kwa maslahi ya taifa, na kwamba lawama zisizo za msingi ni jaribio la kudhoofisha juhudi zake. Alisisitiza kuwa Mbowe ni muhimu kwa chama.
Mbowe ni jabali la siasa za upinzani Tanzania. WanaCCM tutaendelea kumsapoti mzalendo mwenzetu Mbowe kwenye kukijenga CHADEMA. Lissu ni adui wa demokrasia na kirusi ndani ya chama rafiki CHADEMA.
Mratibu wa kampeni za Freeman Mbowe Daniel Naftari amepinga uwepo wa ukomo wa uongozi ndani ya chama hicho kutokana na kile alichoeleza kuwa chama hicho kina raslimali watu wachache (wa kariba ya Mbowe) wenye uwezo wa kuongoza mapambano ya kisiasa hasa kwenye nyakati ngumu
Akihojiwa na Jambo TV, Daniel amesema taasisi ya kisiasa ya upinzani kama ilivyo CHADEMA haiko sawa na taasisi nyingine za kiutendaji kwani, hiyo inahusisha mapambano ya kisiasa ambayo kwa kiasi kikubwa yanahitaji raslimali watu makini na wenye weledi mkubwa wa kuyaendea mambo magumu na kuyatafutia majawabu
"Hii nchi wapo watu wengi wazuri hawapendi CCM lakini wanaamua kwenda kufanya siasa CCM kwa sababu ni rahisi na wanakuwa salama, kufanya siasa za upinzani sio salama, leo mnazungumzia ukomo wa uongozi sio kwamba tuna utajiri wa watu hapana, mnawajadili watu wawili tu hapa Mwenyekiti Mbowe na Makamu wake Lissu , wako wawili tu, hamna upana huo wa raslimali watu"