Watu wengi hapa JF wamekuwa wakiomba ushauri wa namna ya kuanzisha au kuboresha shughuli mbali mbali za kiuchumi. Lakini watu wengi wanaomba ushauri ns wakisha upata huwa hawana kawaida ya kutupa mrejesho wa mafanikio au kutofanikiwa. Sasa ni wakati muafaka kwa watu kutupa mrejesho wa yale walio tushirikisha iliili wengine wajifunze. Kitu ninacho ona hapa nahisi wengi wetu huwa hawamaanishi kile wanachotushirikisha. Wengi wanakuwa ni watu wa keybord tu na siyo watu wa action.