Mrejesho; Biashara ya madini ya dhahabu... fourth season

Mrejesho; Biashara ya madini ya dhahabu... fourth season

mcrounmj

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2016
Posts
380
Reaction score
889
Wakuu, hongereni kwa mapambano ya hapa na pale katika kuutafuta mkate wa kila siku, pengine kutengeneza ziada ya kufaa kesho.

Mniwie radhi kwa kuwa niliahidi kila baada ya miezi sita nitakuwa nadondosha mrejesho wa mahali nilipo katika safari yangu kwenye madini. Nikili tu kuwa mambo yamekuwa mengi mno na muda mwingine najikuta naisahau kabisa jamii yangu ya hapa jf ambayo imekuwa mhimu mno katika mapambano yangu kwa kunitia moyo, kunishauri na kunikosoa pia.

Kama ndio mara yako ya kwanza unaingia kwenye uzi huu naomba niambatanishe link za season zilizotangulia.

First season JamiiForums mobile app
Second season
Third season
Wakuu mpige kambi maana nakuja

Fourth season.

Msimu huu wa nne kwangu ulikuwa msimu wa mavuno. Baada ya kazi ya mwaka mzima wa kusaga na kukusanya mchanga wa dhahabu, hatimae mwezi June nilipeleka plant kuchenjua.

Labda tu nifahamishe kuwa nilibeba gari 30 zenye ujazo wa tani kumi. Sample baada ya mchanga kuchanganywa kwenye ubebaji ilisoma 3.5 ppm. Copper pia ilikuwa inasoma 750. That was not surprise kwa sababu mwanzo nilisaga mawe ya kutoka sehemu tofauti.

Changamoto nilizokutana nazo ni.... Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuchenjua hivyo niliogopa kuibiwa mnoo. Mkemia niliyempata hakuwa competent na hiyo nilikuja kujua tayari tupo mzigoni. Yaani ni kama alishindwa kuidhibiti vizuri copper.

Ila yote kwa yote tulijitahidi na ukubwa au uwingi wa mzigo ukanibeba. Kutoka kwenye makadilio ya kilo mbili....nilipata gram 860. Asilimia pia ilisoma 97. Hapo approximately nilipata kama milioni mia moja na tatu. Ukitoa gharama za uchenjuaji na kulipa vijana wa kazi, inabaki kama milioni sabini

Nilijiona kama nimekosa, maana hesabu zangu zilikuwa kwenye milioni mia mbili plus na nilishawaza kutafuta leseni ya dealer ili ni-trade dhahabu kwenye viwango vya juu zaidi.

Kitu ambacho nimejaaliwa na huwa nakiona kama baraka ni kujiona kwenye nafasi ya ushindi kwa kila ninachokipata haijalishi udogo au ukubwa. Kwangu mimi milioni sabini ilikuwa great reservation. Kwanza kwenye maisha yangu na utafutaji wangu sijawahi kuipata hapo kabla.

Malengo yamefeli.... Milioni sabini haziwezi kuwa dealer. Hivyo nimejenga nyumba ya kuishi standard, pia naendelea na biashara ya dhahabu. Hela nyingi nimeirudisha kazini ambako tayari nakuza mlima. Kiufupi hela ya dhahabu ni tamu mnoo, sijui kama ipo siku nitakuja kuacha shughuli hii.

Nimalize kwa kusema kuwa.... uchimbaji ni kama biashara ya madawa ya kulevya kwa namna hela yake inakuja kwa kasi. Ukiwa serious with a capital within 3 years utakuwa billionaire believe me.

Mungu atujaalie uzima na rehema, tuishi maisha ya ndoto zetu. See you on the fifth season.
 
Nauliza vipi ukadirie kupata 2kg wakati ppm ilisoma 3.5? Kama nipo sawa ulikuwa na wastani wa 300tons za mchanga ambazo kutokana na ppm iliyosoma labda ungepata wastani wa 1kg, Naomba nisahihishe kama nimekosea.

Sent from my TECNO KD7 using JamiiForums mobile app
Lori zitumikazo ni zile za cbm 4-5
Wastani wa tani 5
Kwa hesabu hawezi zidi gram 500
Kwa hiyo aina ya ppm na hizo lori
 
Mkuu ungepitia third season ungeelewa vizuri. Wakati nikiwa nakuza mlima nilipima sampo mara kadhaa, kuna wakati ilisoma 8ppm, 5ppm na 4ppm. Hapo ilikuwa bado sijaubeba mlima. Kwahiyo nikaamini kwa sampo hiyo kilo mbili lazima. Kumbe uchukuaji wa sampo una utaalamu wake ili ukuletee uhalisia. Hivyo makadirio ya kilo mbili ilikuwa kabla mkemia hajachukua sampo.

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Lori zitumikazo ni zile za cbm 4-5
Wastani wa tani 5
Kwa hesabu hawezi zidi gram 500
Kwa hiyo aina ya ppm na hizo lori
Gari zinatumika za tani kumi, ila kulingana na upakiaji mda mwingine zinabeba tani nane

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mcrounmj kwanza hongera sana kwa hatua uliyofikia inshallah utafikia ndoto zako. Kuna mwanangu nae kavuna kiasi kama chako huku huko ulipo, I wonder kama ndo wewe ha ha

Kwa mahesabu yangu naona umepata unachostahili kutokana na rundo ulilokuwa nalo wala mkemia hajakuangusha, in other words you overestimated your calculations.

Tani 30 x 10 = 300.
300 x 3.5ppm = 1050

Kumbuka huwezi vuna zaidi ya 70% kwenye leeching VAT. Na copper yako ilikua ndogo sana which is a very good thing.

So, 1050 x 0.7 = 735. Hizi ndio gram ulizotakiwa kupata, wewe umepata 860 na purity ya 97. That's very high.

Mkemia kafanya kazi kwa weledi wa juu sana, in this business mkemia akikosea unaweza usipate kitu kabisa maana there's no reversing.

Hongera chief.
 
Asante sana chief.... kikubwa nimepata mtaji na uzoefu, expectations zangu ni kufanya vizuri zaidi next season. Over approximation imetokea baada ya mimi kuwa nachukua sampo pale kwenye rundo ikanidanganya. Sampo ya mkemia ilitoa mulemule

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Asante sana chief.... kikubwa nimepata mtaji na uzoefu, expectations zangu ni kufanya vizuri zaidi next season. Over approximation imetokea baada ya mimi kuwa nachukua sampo pale kwenye rundo ikanidanganya. Sampo ya mkemia ilitoa mulemule

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app

Huyo mkemia ni mzuri sana mtumie tena. Kupata zaidi ya 800g ni maajabu.

Unaendelea kusagia watu au unaanza uchimbaji mwenyewe?
 
Mkuu ungepitia third season ungeelewa vizuri. Wakati nikiwa nakuza mlima nilipima sampo mara kadhaa, kuna wakati ilisoma 8ppm, 5ppm na 4ppm. Hapo ilikuwa bado sijaubeba mlima. Kwahiyo nikaamini kwa sampo hiyo kilo mbili lazima. Kumbe uchukuaji wa sampo una utaalamu wake ili ukuletee uhalisia. Hivyo makadirio ya kilo mbili ilikuwa kabla mkemia hajachukua sampo.

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
Ahsante kwa ufafanuzi, tupo wote kwenye sekta. Allah akutimizie ndoto zako, Aamiin.

Sent from my TECNO KD7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom