Mrejesho (feedback): Nina Shilingi Laki moja na nusu, ni mwanafunzi, naweza fanya biashara gani?


Umefanya vizuri kurudi jukwaani kushukuru, hawa sasa ni ndugu zako,wala hawatakuchoka, na pengine leo wamefurahi kuona michango yao imejibu. Nitakupa ushuhuda wangu.

Mzee mmoja alinisaidia,niliona aibu kurudi kushukuru sababu nilikuwa apeche alolo,ila aliniusia kuwatendea wengine vizuri. Miaka imekatika mingi,mwaka juzi nilifanya kazi ya uwekezaji ya dada mmoja vizuri. Mwaka jana mwishoni ndio nimekuja kugundua, yule dada ni mjomba wake na yule mzee aliyenisaidia. Mzee aliniinua mimi na mimi nimekuja kumlipa yeye bila kujua kama narudisha fadhila zake. Hata kama huna kitu na ukawa na dhamira safi Mungu anaona, wewe shukuru tu.
 

Safi sana Mkuu.
Nakushkuru kwa sababu umeleta feedback ambayo sio kwa nia ya kushukuru tu bali pia imekuwa kama motivation na inspiration kwa wengine.

Mungu akuzidishie.. InshaAllah
 

Wow!
Ahsante sana ndugu Malila
 
Last edited by a moderator:
Safi sana Mkuu.
Nakushkuru kwa sababu umeleta feedback ambayo sio kwa nia ya kushukuru tu bali pia imekuwa kama motivation na inspiration kwa wengine.

Mungu akuzidishie.. InshaAllah

Ahsante sana Bw.Daffa
 
Last edited by a moderator:

Hongera sana kaka
 
Hongera sana mkuu!,Ila ungeweka mchanganuo japo kwa kifupi jinsi biashara ulivyoifanya ingeleta faida kwa mwana jamii mwingine pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…