Mrejesho: Matokeo ya kilimo cha alizeti Singida

Ibravo

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
539
Reaction score
202
Habari Wanajamvi,

Baada ya kujiunga JF si muda mrefu sana nimepata fursa nzuri ya kuweza kupitia threads mbalimbali hasa za ujasiriamali zilizonipa hamasa za kuchangamsha ubongo wangu kipi cha kufanya maana kuna mambo mengi sana yameongelewa na bado mengine mapya yanazidi kuongelewa.

Maamuzi niliyoyafikia ni kujaribu kilimo cha alizeti huko mkoani Singida,kwa nini basi ni Singida na si mikoa mingine?
Kwanza ni mkoa kati ya mikoa mingine unaokubali sana zao la alizeti,pili usimamizi kuwa rahisi upande wangu kwani kuna mwenyeji wangu huko Singida anayenisimamia kilimo hicho.

MREJESHO
Niliamua kuanza kulima kwa kujaribu hekari 2 maana ndio ilikuwa mara ya kwanza kuanza kilimo,taarifa nilizopewa na mwenyeji wangu ni kwamba hekari 1 ingeweza toa gunia 8-10 kutegemeana na rutuba ya udongo na hali ya hewa kipindi cha kilimo.

Kukodi hekari 1 kwa kilimo kwa miezi 6 ni 30,000/=, kuandaa shamba pamoja na kupanda kwa heka 30,000/= ,palizi kwa heka 20,000/= na ni mara moja tu, kwa hiyo hekari 2 zilinigharimu takribani sh.160,000/= za kitanzania.

MATOKEO
Kwa kweli nilichokipata sijakitegemea maana mipango yangu mingine italazimika kusimama kwa muda.

Hekari ya kwanza kuvunwa zimepatikana gunia 2 na debe 3 za alizeti, hekari nyingine gunia 3 na debe 2 jumla gunia 5 na debe 5, kwa kweli matokeo haya yamenivunja moyo mno.

Hvi sasa kwa taarifa nilizozipata ni kuwa gunia 1 la alizeti linauzwa kati ya sh 40,000-45,000.

MATARAJIO YANGU
Ninachotarajia ni kuendelea tu na kilimo ingawa msimu huu umeenda ovyo sana. Ninajipa moyo kwani nikiamua kuuza alizeti nilizozipata nitaweza japo kurudisha gharama nilizozitumia ktk kulima,naamini kuweza kurudisha cost nilizotumia ni bora kuliko kukosa kabisa kwani hata hivyo nimepata angalau uzoefu kidogo kwa kujaribu.

NILICHOJIFUNZA
Alizeti haitaki maji mengi sana, hii ni moja ya sababu iliyochangia kupata gunia chache, maana mwaka huu mvua nyingi sana imenyesha huko Singida na hata hapa Dar nimeliona hilo.

Uchaguzi wa mashamba ya kulima, ili uweze kupata matokeo mazuri inatakiwa uchaguzi mzuri wa shamba,upande wangu nilichelewa sana kutuma pesa hivyo mashamba mengi yenye rutuba yaliwahiwa na wakulima wengine.

N.B Sikutumia mbolea wala kitu kingine zaidi ya kutegemea rutuba ya udongo, ninaamin nayo ilichangia kwa matokeo haya mabaya.

MAAMUZI YANGU
Ni kutokata tamaa wala kushindwa maana nimejaribu na naamini ninaweza na nitaweza tu, siku zote najua kuwa unapopata tatizo ama matokeo mabaya kama haya cha kwanza ni kujua sababu (Causes) zilizopelekea matokeo hayo(Results),hata mwanamke akikumbia jaribu kutambua sababu zilizomfanya akukimbia ili hata mwingine utakayempata uweze kuzuia udhaif wak na si kuendelea tu kuhangaika kutafuta mwanamke mwingine bila kujua wa kwanza alikukimbia kwa sababu gani.

Ntaongeza idadi ya heka angalau heka 5 nione nitakachokipata,malengo yang ni kuongeza idadi ya heka kila mwaka wa kilimo hadi ntakapoona mafanikio mazur.

HAYO NDIO NILIYOYAPATA HUKO.

Nakaribisha Michango Yenu Ama Ushauri.

Asante JF..!!!!
 
Thanx!
Nitaendeleza Juhudi Bila Kujali Vizingiti Mbele Ya Harakati Hizi Za Kujikwamua Kutoka Ktk Wimbi La Umasikini.
 
Hongera sana mkuu!,. Usikate tamaa mwaka fanyia kazi uliyojifunza. Naamini mwakani lazima utatoboa.
 
Hongera sna,maelezo yako yanaonyesha kwamba ulichelewa kupata mashamba mazuri napia inawezekana hata kuchelewa kupanda ulikuwepo,napia yawezekana usimamizi hakuwa mzuri yani kazi haikufanyika kwa mda muafaka.unapopanda mmea haikusubiri wenyewe unaenda nakumbizana na mda ukishafika mda wake km haukuzingatia kanuni zake ndyo unambulia less production.
 
mkuu usiwe na haraka kuuza hayo mazao mwezi wa 12 hupanda hadi 90000 kwa gunia kama una haraka hapo sawa
 
Pia jitahidi unapolima usisubiri kuangaliziwa kila wakati,unatakiwa na wewe upate muda wa kwenda kucheck hali inavyoendelea na kuona hali ya mazao yako ikoje.
 
Mh GEBA nilichokifuata ni kusikiliza kwanza ushauri wa wenyeji kupata fununu za awali,kwan ni mgeni kuhusu kilimo na hata maeneo yenyewe so ni bora kusikiliza wenyeji kwanza.

Kitonga vs Sekenke kuhusu kufuatilia mwenendo mzima nimepanga ntakapo lima hekari nyingi zaidi hata hizo 5 nilizoplan msim unaofuata kwan gharama zitakuwa kubwa so uangalizi muhimu sana
Asanten kwa mawazo yenu.
 
Hayo mashamba yapo Singida kijiji gani au sehemu gani?
 
shida ni mtaji tu hapa tz.................. ungekua na 5m ungetoka rasmi
 
Kwanza hongera kwa kuthubutu.
Pili, ningekushauri kama mkakati wa muda mrefu uanze kutafuta eneo lako ili liwe la kudumu, kisha uwaone wataalamu wakupe mbinu namna ya kuboresha udongo ili uwe na rutuba kwa muda mrefu, kisha mambo mengine yatajipa.
 
Mmmh! Hongera kwa kuthubutu!! Nnampango wa kulima vitunguu huko ngoja nifanye utafiti kwanza!!
 
wakati wa mavuno ulikuwepo au ulivuna kwenye simu?
 
Haahaaha eti ulivuna ktk simu!!Mambo ya Dijitali haya
Tangu mwanzo wa mavuno nimemtuma wife maana ndio kwao huko Singida so taarifa zote nazipata toka kwake,hawezi iba kwan akiiba atakuwa anajiibia mwenywe pesa toka mfuko wa dela kwenda ktk tight aliyoivaa.
 
shida ni mtaji tu hapa tz.................. ungekua na 5m ungetoka rasmi

angekuwa ni hiyo 5m wakati anaanza ndiyo angepotea kabisaa! hivyo alivyoanza ameanza vizuri sana, ameanza kidogo kitu na amepata darasa la bure, next time anaweza kupanua shamba na kurekebisha makosa na akaendelea, akishakuwa confortable sasa anaweza kuwekeza pesa nyingi! kilimo cha kutegemea mvua siyo cha kuchezea hata kidogo, kinaweza kukutoa au kukuondoa kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…