Mrejesho: Mtoto hapati choo

Mrejesho: Mtoto hapati choo

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
refer threadhttps://www.jamiiforums.com/threads/mtoto-wangu-hapati-choo-vizuri.1415871/
nashukuru sana kwa ushauri wenu
tulizingatia ushauri ufuatao na mtoto anapupu kila siku sasa tena kinyesi cha kutosha

PyaarJF-Expert Member
#15
Sunday at 2:18 PM

Joined: Feb 11, 2018
Messages: 1,121

Likes Received: 3,609

Trophy Points: 280
Kwa mtoto mdogo kupitisha siku 2-3 bila kupata choo si kawaida, kutakuwa kuna shida kidogo.

A) Kwa mtoto anayenyonya.
Unatakiwa ujue kama mtoto ananyonya vizuri, vile vile uzingatie hali ya lishe ya mama kwasababu hiyo ndo huchangia kwenye kutengeneza maziwa ya mama.

Kwa kawaida kiafya mtoto anatakiwa anyonyeshwe dakika 20 ziwa moja. Kwasababu unyonyaji wa mtoto dakika 10 za mwanzo kinachotoka ni maji kwa wingi pasipo kuwa na nutrients za kutosha kwenda kwa mtoto, dakika 10 zinazofuata ndo kunakuwa na nutrients za kutosha.

Akina mama walio wengi hawafuati/hawajui utaratibu huu hivyo kupelekea mtoto kuhamishwa hamishwa manyonyo hata kabla ya dk 10. Hivyo kupelekea mtoto kupata maji ziwa hili na kumalizia kupata maji ziwa lingine, anakosa virutubisho vya kutosha, hivyo kupelekea shida katika upatikanaji wa choo.


Endapo mtoto ananyonya vizuri na tatizo likaendelea kuwepo kuna uwezekano mkubwa kukawa na shida katika mfumo wa chakula (Mara nyingi tumbo linakuwa kubwa na anaweza kupata maumivu makali ya tumbo.

B) Mtoto anatakiwa apewe chakula chenye nyuzinyuzi (fibres) kwa wingi, ambavyo ni pamoja na:-
-Matunda
-Mboga za majani
-Maji ya kunywa ya kutosha.
Inashauriwa mtoto mwenye mwaka 1-2 anywe lita 1.3 kwa siku.
-Vyakula vyenye maji maji.

Hivyo basi jaribu kuangalia wapi haupo sahihi katika lishe ya mtoto ili urekebishe. Endapo tatizo litaendelea jaribu kufika hosp. kwa uchunguzi zaidi.
 
Asante sana nina mtoto mdogo nimejifunza kitu hapa
 
Back
Top Bottom