MREJESHO NA USHAUR WENU WAHITAJIKA

MREJESHO NA USHAUR WENU WAHITAJIKA

scientificall

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2015
Posts
457
Reaction score
328
Zimepita wiki mbili toka nilete uzi kuhusiana na kesi ya kusingiziwa wizi na mshitaki wangu kulazimisha nimlipe hata nusu ya gharama ili kesi iishie polisi.

Kutokana na kuwa na ndugu huko polisi mshitaki wangu alinisumbua sana kwani nilikuwa nikidhaminiwa nakamatwa tena kwa amri ya R.C.O wa mkoa kutokana na ndugu zake huyu mshitaki kujuana na R.C.O.

Baada ya kuhangaika hapa na pale nilifanikiwa kutoka central na kwenda mahakamani kwani R.C.O alimwagiza askari mpelelezi wa kesi yangu aniwekee pingamizi la dhamana mahakamani kwakuwa nmegoma kukiri kuiba computer.
Lakini Mungu mkubwa tulivyofika mahakama ya mwanzo askari alikubali nipewe dhamana na nikadhaminiwa.

Tukirudi huku uraiani ni kwamba aliyenshitaki mpaka mda huu amekosa mashahidi kwani majirani wote wanakataa kuwa mashahidi wake wakidai hii kesi ni ya kusingizia na haina ukweli ndani yake.
Kutokana na maelezo yaliyotolewa tofauti na mshitaki wangu polisi na kwa uongozi wa chuo ambaoyo ni.

1.Alivyohojiwa na uongozi wa chuo (dean of students)ailidai....."mnamo saa saba usiku aliskia upepo unasukuma mlango na baadae akaona dirisha linafunguliwa na kushuhudia mkono wa mtu ukichukua simu, na kurudia simu ya pili, na baadae ukichukua computer mezani.

Mwisho wa tukio alivyokuja kuchungulia dirishani akaniona nimesimama pembeni natoa maelekezo. Hapo ndipo alilala na kuja kustuka asubuhi saa moja na nusu na kutoa taarifa kwa majirani."

2. Maelezo aliyoandika polisi..... "Mnamo saa saba usiku alifungiwa nje na wezi wakaanza kumuibia kupitia dirishani na alipo chungulia akaniona mimi kwa mbali nakimbia na mali yake."

Siku ya kusomewa shitaka mshitaki wangu hakuwepo na hakimu alinisomea makosa 2.
1. Kuvunja kwa nia ya kuiba.
2. Kuiba mali.
Mashitaka yote nliyakana na ikatajwa tarehe ya kusikiliza kesi.
Kwa upande wangu mshitaki hakunikamata na kidhibiti chochote lakini pia computer yake anyodi iliibiwa kupitia dirishani haiwezi kupita pale dirishani na majaribio yamefanyika.

Lakini pia mimi ninae mdogo wangu nlielala nae na siku hio sikutoka nje.

Ushaur wenu je hii kesi ntaishinda au itakuwa na mkono wa rushwa.
 
Pole sana usife moyo kesi hiyo utashinda tena mapema tu wala huhitaji mawakili kukusaidia kikubwa jiamini na uwe na uhakika wa unachokisema
 
Back
Top Bottom