Mrejesho: Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2016
Posts
4,707
Reaction score
11,365
Salama wakuu.

Miezi kama mitano nilikuja hapa na thread hii hapa chini.

Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba. Nawe waweza jaribu mahali unapoishi

Ingawa nimepata faida ya kutosha mpaka sasa lakini nilitaka nibadilishe au nipanue biashara yangu kidogo.Katika biashara nilizotaka nifanye ni hizi hapa chini.Nimeamua nibadili aina hii ya biashara ili niweze pia kumsomesha mdogo wangu wa amekosa mkopo.

Ningeomba mawazo yatakayotolewa yajikite katika biashara hizi tatu,nisingependa mtu atoke nje ya biashara hizi tatu.

1.Ninunue boda boda mbili niwape watu wasimamie kisha watakuwa wananiletea elfu 22 kwa siku.

2.Nifungue saluni BABER SHOP ya million 4(kwa siku hapa nipewe tu elfu 15)

3.Au nifungue kiduka cha rejaleja cha mtaani cha million nne(changamoto hapa nikumpata muuzaji muaminifu) hapa pia ntaendelea kufanya biashara yangu ya mchele.

NOTE:
Pesa niliyonayo mpaka sasa ni 4m Baada ya kupata msaada wa member mmoja wa Jf wa Million moja baada ya kutembelea na kuona biashara yangu.
 
Fungua kiduka m1
Kinyozi m1
bodaboda m1
Iliyobaki itakuwa inazilinda biashara panapo mapungufu
Mkuu kiduka cha milioni moja sidhani kama kinawezekana labda ungedadavua kiwe cha aina gani.

Hakuna boda boda mpya ya 1M.

Pia saluni ya 1M itakuwa saluni ya aina gani mkuu,kama tu machine moja ya saluni ni laki na ishirini.

Bado vioo,kiti cha kukalia.Sehemu ya mtu kuoshwa akimaliza sheviwa.Mkuu miioni moja haitoshi kwa saluni nayoihitaji.
 
Kiduka fungua (genge duka) uswahilini hiyo pesa ni nyingi mno na inabaki....kila siku sales waweza pata si chini ya laki
Saluni usitake za ufahari muhimu ni usafi....
Boda boda nunua second hand au nunua mpya kwa 1.5
 
Mkuu samahani kwanza
Nataka kufanya biashara ya mchele, unaweza kunipa uzoefu?
 
Kiduka fungua (genge duka) uswahilini hiyo pesa ni nyingi mno na inabaki....kila siku sales waweza pata si chini ya laki
Saluni usitake za ufahari muhimu ni usafi....
Boda boda nunua second hand au nunua mpya kwa 1.5
Umesomeka kiongozi shukrani.
 
Nataka kufanyia arusha au Dar?
Wapi pana soko zaidi
Kimakazi nakaa arusha ila nipo dar saa hii
Mimi binafsi nimefanyia Dar kuhusu arusha kiukweli sifahamu,Dar kuna soko zuri ila sifa ya watu wa dar wanataka mchele ulionyoka pia wenye harufu.Ukitaka mchele wako uuzike basi uutoe kyela au Shinyanga pia mchele wa Tabora mzuri hauna tofauti na Shinyanga ila ukisema wa tabora wengi wao hawanunui.
 
Fungua barbershop uweke na mdada mzuri wa kufanyia watu massage. Pia ubuni kitu kitakachokuwa kinawavutia watoto kungangania wazazi wawalete wanyolewe hapo, italipa sana.
 
Biaahara zote zina changamoto hapo, lakini ngoja nikupe baadhi ya Facts.

1/BODA BODA.
Hesabu ya kawaida kwa sasa ni kati ya Shilingi Elfu Tano mpaka Elfu saba kwa siku. Ni vigumu sana kupata maeneo ambayo unaweza ukapata Elfu kumi au zaidi kwa Siku.
Changamoto kubwa sana ipo kwenye Usimamizi, vijana wengi wa Boda boda vichwa vyao vinashika moto, Kukuharibia pikipiki, kushindwa kuleta hesabu, ajali, kukamatwa na Polisi nk. ni mambo ya kawaida sana kwao. Kifupi kufanikiwa katika biashara hii kunahitaji upate dereva mwaminifu sana au uendeshe mwenyewe!
Ushauri wangu, tafuta kwanza uzoefu na fanya utafiti wa kina katika eneo husika kabla ya kufanyaa biashara ya Boda boda, na ikiwezekana uanze na pikipiki moja badala ya zote mbili.

2/Barbar Shop(Saloon ya Kunyoa).
Ni biashara inayolipa vizuri lakini yenye changamoto hizi.
-Eneo unalofanyia biashara hii(Ukikosea katika hili, basi faida sahau).
-Mtaji wa kutosha (Saloon ya kisasa inahitaji vifaa vingi na vya kisasa plus marekebisho ya mara kwaa mara kwa sababu ya uchakavu).
-Kinyozi mzuri mwenye Ujuzi wa kunyoa, Tabia njema, usafi, Ustaarabu na huaminifu(Hapo ndipo kimbembe kipo hasa)

3/DUKA.
Hii ni biashara ya uhakika zaidi, yenye uwezekano mdogo sana wa kufilisi mtaji ikitokea biashara imekuwa ngumu. Changamoto..
-Utakuchukua muda zaidi kuweza kuchanganyia kupata wateja ili uweze kuona faida yake hasa. (Unaweza kusugua hata mwaka mzima bila kuwa na wateja wa kutosha wa kuweza kukupa faida)
-Haihitaji haraka kuweza kupata faida.(Uvumilivu ndio siri ya kufanikiwa katika biashara ya duka)
-Faida inategemea sana na Maeneo ambayo duka hilo lipo. Mitaa yenye uwingi wa watu ndio eneo sahihi zaidi kwa biashara hii.
-Faida yake inategemea Muuzaji wake. Kumwajiri mtu akuuzie duka ni mtihani mkubwa sana katika biashara hii. Uwezekano wa faida yote kunyonywa ni mkubwa sana.

Kwa leo naishia hapo!!!
 
Fungua barbershop uweke na mdada mzuri wa kufanyia watu massage. Pia ubuni kitu kitakachokuwa kinawavutia watoto kungangania wazazi wawalete wanyolewe hapo, italipa sana.
Mkuu kiukweli kwa saluni ninayoitaka kuhusu muundo wake utakua mzuri tu.Pia mpaka sasa nipo mkoani kuna kinyozi mmoja nimemuona na nimemuuliza kama akipata maslahi yakutsha dar anaweza kwenda piga kazi kakubali.Lakini sasa nilitaka nimawazo ya wadau wengine maana penye wengi hapaharibiki kitu.Kuna watu niwazoefu sana wa hizi kazi nilitaka nao nione michango yao.
 
Mkuu nakushauri ungeongezea mtaji kwenye biashara ya mchele ambayo unaimanage vizuri, kikubwa unachoweza kufanya ni kuongeza soko la bidhaa zako, naamini kwa kuweka namba zako humu utapata wateja wengi zaidi. Hizo idea za biashara unazotaka kuzifanya sio mbaya kama utakua na usimamizi wa karibu ila hazina faida kama hazina usimamizi wa karibu sana(sababu kubwa ni uaminifu, hatuna watu waaminifu katika familia zetu kwa sasa). Ila nafaka ni biashara nzuri na rahisi kuimanage. Sana sana unaweza kuongeza bidhaa nyingine tofauti za nafaka, kama maharage, ulezi n.k
 
Mkuu asante kwa mchango wako nimeusoma nakuelewa vizuri,nimeondoka nakitu hapa.
 
Mkuu asante sana ushauri wako naufanyia kazi,pia kuhusu wateja wa humu JF nimepata aisee sihaba.

Lakini tatizo lakutaka kumuweka mtu nikuwa sasa naingia mwaka wa tatu course yenyewe ni ngumu Mechanical eng ndio maana nilikuwa nataka nifanye biashara ambayo sintoisimamia sana.Pia nilitaka nichangie kumsomesha dogo maana hali mbaya hom ingawa kafauru vizuri na course yake priority lakini ndio hivo mkopo hamna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…