Ryder2
Member
- Sep 11, 2021
- 81
- 88
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, kwa kifupi nimekua nikitumia beta blocker kwa takriban inaelekea kufika miezi 8 hivi na baada ya muda kidogo kuringana na ushauri wa doctor kwa kuniambia niache kutumia hizi dawa beta blocker (NEBIVOLOL 5MG TAB), hivyo nikaona sio mbaya kuziacha nikajaribu bahati yangu kwani nilifanikiwa kuziacha hizi dawa kwa muda wa takriban week 3 na siku kadhaa ila muda huo nilishapunguza dozi hivyo dozi nilikua natumia kipindi hicho ni NEBIVOLOL 1.25MG ( ROBO KIDONGE).>>HABARI ZA MUDA HUU WAKUU!
Kuacha kwa hizi dawa kuliambatana na madhara mengi sana yakiwemo
- Kizunguzungu kikali sana
- Mwili kuishiwa nguvu
- Kukosa concentration na balance ya mwili
- Mapigo ya moyo yalipanda zaidi ila kwa usiku yalikua yanatulia
- Mikono kua ya baridi na miguu
- Kuchoka sana
- Presha pia ilikua abnormal ila nilicontrol kwa kula ndizi na machungwa.
> Muda ulienda ndipo nikaamua kuwasiliana na dokta wangu wa magonjwa ya moyo na tukakubaliana na tarehe ya Vipimo vya ECG na ECHO na majibu yakawa kama ifuatavyo:
ECHO: Kipimo kilisema ESSENTIALLY NORMAL ECHO FINDING'S yani
- ALL VALVES ARE NORMAL IN STRUCTURE AND FUNCTIONS
- NORMAL SIZED CARDIAC CHAMBERS
- LV- UNIFORM CONTRACTILITY
- NORMAL SYSTOLIC FUNCTION WITH LVEF 64.38%
- NORMAL DIASTOLIC FUNCTION
- IVC-NORMAL, NO SHUNT/THROMBUS , NORMAL PERICARDIUM
HAYA MAJIBU HAYANA TOFAUTI NA YALIOPITA ISIPOKUA KWENYE LVEF MWANZO ILIKUA LVEF 71% BUT NOW IMESHUKA HADI LVEF 64.38% (HAPA NAONA KUNA IMPROVEMENTS KIDOGO)
KUHUSU KIPIMO CHA ECG NACHO KWA SASA KIMESOMA SINUS ARRYTHMIA ( BORDERLINE ABNORMAL ECG)
Ambapo kulingana na maelezo ya dokata anasema sinus arrythmia sio ugonjwa wa moyo ni hali tu huwa inawatokea watu na upotea kadri umri unavozidi kusogea( old age) na haina madhara yoyote yale kiafya.
Ila dokta ameshauri niendelee tu na hizi dowa kwa dozi ndogo tu mambo yatakua mazuri tu hapo badae
HITIMISHO: Nimejifunza mengi sana kuhusu hili tatizo na maajabu kwetu hakuna mtu mwenye ugonjwa wa moyo wala magonjwa chronic yoyote ila ndo hivyo tu may be Mungu ndo kanipa mtihani wangu hapa duniani hivyo inabidi niishi hivyo.
TUMRUDIE MWENYEZI MUNGU KWANI KWAKE HAKUNA KINACHOSHINDIKANA