Habar zenu wakuu!
Naitwa Aleyn, nipo hapa Jf toka 2011 ila nimeijua JF toka 2009. Leo ninaleta kwenu mrejesho jinsi nilivyofanya surgery ya macho makengeza.
Nitaandika kwa kukatisha katisha vipande sababu mimi sio muandishi mzuri.
... 2010 nikiwa seblen natazama picha zangu ambazo zipo seblen naona picha ya kwanza nikiwa mtoto mdogo kabisa kama wa mwaka mmoja hivi, sikujiona kama nna macho makengeza. Picha ya pili kuitazama ni ile ambayo nikiwa secondary form 2, nikitazama nkajikuta sikuwa na makengeza kama ambayo nilikuwa nayo muda huo 2012.
... 2012 nikapost Jf na kuwatafuta watu mashuhuri wa tiba JF akiwemo mwanakijiji sijui mti mkavu, ni maarufu humu ndan kwa mambo ya tiba za asili, baada ya hapo nikawasiliana na Doctorz ambao walipost ktk ile thread. Wote wakanambia hakuna dawa so niridhike na vile ambavyo nilivyo, Yes nikaamua kutofatilia kbs hii ishu, ikawa kila nikienda kusali nilitegemea muujiza tu siku Mungu aniponye kwa namna yake.
... Moja ya vitu ambavyo nilikuwa siviwezi ni kupiga picha, kila nikijitazama baada ya picha nilijisikia vibaya mno, au nikiwa navaa kisha najitazama ktk kioo nilijiona niko vibaya sana ktk macho yangu.
... 2018 nikiwa kazini tukatembelewa na dokta flan hivi, jamaa anasomea udaktar bingwa wa macho na anafanya kaz pale MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL, nikajikuta tu nimemwomba kuongea nae faragha, akakubali na nikamueleza shida yangu, akacheka mno akasema mbona makengeza yanatiba kwa njia ya surgery? Akauliza una Bima? Nkamwambia NO. Akasema tafuta Bima kisha uje MNH.
... Baada ya hapo ikabidi nizame JF, baada ya kuzama nikaona posts na thread kadhaa watu wakisema MNH na CCBRT wanatibu hii ishu.
... Nikapata aman kubwa mno, aman kubwa saaana. 2020 nikajaza form za bima na 2021 nikapata bima yangu rasmi. Nikajaribu kutazama hospital ipi niende, nkaona CCBRT haina mambo mengi. Nikazama pale CCBRT, nikakutana na Dr mmoja mrembo wa kihindi, umri wa makamo anaitwa Dr. Sonia. Alinifanyia vipimo vyote, then akaniuliza unatakaje? Nkamuulza ww unaona nawezaje nkawa sawa? Akasema ni surgery, moyon nikasema Good sababu ndicho haswa kilichonileta hapa, baada ya apo akanpost wa specialist wa macho tena, nilipofika pale nikamwambia nahitaji surgery, akanipost kwa Dr wa upasuaji kitengo cha macho, kumbe ni yule yule Sonia.
... Nikaenda kuchukua tarehe yangu ya operation, nilivyochukua nikarud zangu hom, nikashirikisha watu wangu wa karibu wachache mno. Ndugu wengi waliogopa ila marafiki wakasema nenda kafanye, nikatafuta na marafik zangu ambao ni madokta wakasema nenda kafanye.
... Nikaenda zangu kufanya operation, kwa sasa nina mwez mmoja toka nifanye operation. Kengeza limetoka 75 mpka 18, kuna zoez nimepewa la kufanya ili kupunguza iyo 18.
Nichukue nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kuniponya kufikia hapa, kwani amenijibu kwa namna yake. Nishukuru Taasisi ya CCBRT, lakini vile vile kongore kwa JF. Hii site naipenda mno yaani, Mungu awabarik nyote.
Huu ndo mrejesho wangu kwenu, najua wengi wanataman kujua mengi juu ya jambo hili ndo maana nimeleta ushuhuda huu kwenu.
Kama kuna swali lolote uliza hapa chini, NINAAHIDI KUJIBU.