Mrejesho: Nina miaka 26 sasa nimepambana vya kutosha bila ya mafanikio

Hallah

Member
Joined
Aug 29, 2019
Posts
36
Reaction score
43
Natumaini hamjambo,

Mnamo tarehe 30/08/2019 nilipost ujumbe wenye kichwa cha habari kama kinavyosomeka hapo juu

Kwanza kabisa natanguliza shukrani kwa wale waliokuja PM kwa nia njema ya kunisaidia na bila ya kusahau na hata wale waliousoma na ku-comment ujumbe wangu

Wengi walikuja kwa lengo la biashara ya genge na mimi nikajaribu kudadavua yale ninayoyafahamu na kutoa michanganuo mbalimbali kuhusu biashara hii

Pia wapo walioniaminisha kwa kunambia nitafute eneo la biashara na kuahidi kuja home ninapoishi ili tufahamiane

lakini mpaka sasa ninavyoandika mrejesho huu hakuna yeyote yule Niliyefanikiwa kuonana nae wala kupata msaada kwa kile walichoniahidi hasa kuhusu biashara ya genge yaani namaanisha wameingia mitini

Guys naomba tuwe serious yaani mtu anakuahidi anakuja home mwisho wa siku haonekani anajaribu kutoa ahadi siku nyingine tena namsubiri home siku nzima pia haonekani na bila ya kutoa sababu

Kwa kweli ninashida sana na kazi ili niweze kukamilisha malengo yangu

Nimezunguka maeneo mbalimbali kwa lengo la kutafuta kazi lakini nimeishia kuombwa pesa ili niweze kupata kazi

Kesho j3 nitaanza tena kiguu na njia kwa ajili ya kujaribu tena kutafuta kazi maeneo mbalimbali

MBARIKIWE
 
Mimi in kijana wa kiume umri miaka 26 na ni mkazi was Dar es salaam elimu yangu ni kidato cha sita nimeshindwa kuendelea na elimu ya juu kutokana na ukata unaoikumba familia.

Sina mtoto na bado naishi nyumbani napambana kusaka tonge kwa ajili ya familia nafuu yangu ni baba kujenga kibanda hapa mjini nitazunguka lakini mwisho wa siku Nina mahali pa kuweka ubavu wangu

Ni miaka 3 sasa toka nihitimu kidato cha sita nipo mtaani nikijichanganya katika shughuli mbalimbali za kutafuta pesa huku nikiamini siku moja nitadunduliza ili niweze kupata mtaji wa biashara ili niweze kurudi shule

Nimeshawahi kufanya kazi za usafi kwenye makampuni mabalimbali na kwenye hoteli hivyo ninauzoefu wa kutosha kwenye hii kazi

Pia nimeshawahi kufanya kazi ya kuosha magari na kazi ya kupaka rangi nyuma japokuwa sina uzoefu na kazi hizi lakini vipo vipo viwili vitatu ninavyovifahamu

Na pia nimeshawahi kufanya biashara ya genge hii biashara ina lipa sana kama ukipata location nzuri na ukijua kutumia vizuri pesa bila kuigusa pesa ya mtaji kilichoniangusha mmiliki wa biashara alikua na matumizi mabaya ya pesa

Hivyo nimekuja kwenu nahitaji msaada wa kazi ya aina yoyote iliyo halali ambayo haitahatarisha usalama wangu na afya yangu

Pia kama kuna yeyote anahitaji msimamizi wa biashara ikiwa ya genge au duka nipo tayari Mimi si mtu wa starehe na wala sipo interested sana na mademu

Sijui hatma ya maisha yangu na umri unazidi kwenda kama kunayeyote aliyeguswa na yupo tayari kunisaidia namkaribisha PM

NATANGULIZA SHUKRANI
 
Bila shaka nimeambatanisha vibaya ujumbe uliopita na huu wa sasa

TAFADHALI NAOMBA MNIWIE RADHI KWA HILI
mimi ni new meber hapa jforum bado najifunza
 
Daha! Aisee we pambana tu ipo siku utafanikiwa
 
Jomba hata kusoma kwako wazazi wako walipoteza hela bure

Yaani unanguvu, akili timamu , huna ulemavu alafu inakuja kuomba omba huku...

Hivi wabongo ni Nani Alie tuloga? Alafu bado kunawatu wata muonea huruma huyu mtu...

Ndani ya miaka 3 umeruka ruka kufanyakazi sehem zaidi ya 4 na kote umetoka kapa hujioni Kama una matatizo wewe

Kwanza inaonyesha wewe sio mvumilivu na mtu ambae sio mvumilivu ni ngumu kuaminika

Komaa sehem moja mpaka uone matokeo chanya acha kurukaruka
 
Achana na mambo ya kutafuta kazi, kwa Tanzania jikite kwenye kilimo, nenda wanakolima kilimo cha umwagiliaji kodi shamba na anza kulima. Au nenda Njombe, Iringa au Mbeya nunua shamba anza kilimo cha parachichi na miti ya mbao nakuhakikishia baada ya miaka michache ijayo utakuwa kati ya watu matajiri.
 
Ahsante mkuu,
ila huo mradi unahitaji pesa na mimi hata pesa ya kuanzisha biashara ya karanga sina ninachopigania kwa sasa ni kibarua ili niweze kudunduliza na kupata pesa ya mtaji
 
...Sasa wewe 26 years huna hata laki,
Unapoteza muda duniani.

Uza hata mayai ya kutembeza bebq Trey 4 mtaa kwa mtaa kama . sivyo ukifika 30 hutakuwa huna chochote cha kujivunia kwenye dunia hii ya matajiri vijana.
 
Hivi watu munaoandikaga hivi munafikiri ukitaka kwenda kwenye Kilimo basi mbingu inatoboka inakumwagia pesa zakwenda kuanzisha...unaona mtu hats 10,000/= hana then unamwambia aende sijui kufanya kilimo cha umwahiriaji.
 
Anza hata nakuokota makopo Kama huna mtaji!!

Au Chuma chakavu,,au nenda kwenye ma car wash,,,,

Ukifikiria kisomi somi lazima ukate tamaa!!!!
 
You look and sound lazy...mda na resources unazopoteza kuomba omba JF ungezitumia kufanya mambo mengine

Sent from my SM-A510F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…