MREJESHO: Ushauri Gari yangu haichanganyi speed mwisho 60km/h

MREJESHO: Ushauri Gari yangu haichanganyi speed mwisho 60km/h

ndama1

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
278
Reaction score
96
Ndugu wana Jf napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale members wote waliotoa mchango wao wa mawazo, elimu, ushauri atimae nimefanikiwa kusolve tatizo LA gari yangu.

Gari yangu in Toyota Voltz tatizo lake kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza.

Kwa awamu ya kwanza kabla sijaomba ushauri humu Jf nilienda garage zile za mtaani chini ya mwembe wakachokonoa gear box ikawashinda wakatoa recommendation kuwa gari imeuwa gear box hivyo ninunue mpya. Ndipo nikaja humu Jf kuomba ushauri nikashauriwa gari ikapimwe.

Baada ya kuipeleka kwa wataalam wa gear box ILALA DAR wakagundua gear box ni nzima ila mafundi wa mtaani wameichokonoa ikawashinda kuirudishia, Tatizo ilikuwa ni Sparc plug zilikuwa azichomi, Fuel filter ilikuwa chafu na kingine ilikuwa sensor. Hvyo nikasolve tatizo kwa gharama ya kawaida kabisaa gari imerudi mpya.

Ushauri wangu kama unatatizo kubwa kwenye gari hasa izi Automatic ishu za gear box au engine usiruhusu gerage za mtaani wafanye kaz utakuja lia asanteni sana.
 
NDAMA 1 Ilala sehemu gani mkuu?
Ukiwa umetokea buguruni Kwenye makutano ya ilala boma shuka na Barabara inayoelekea kwenda kukutana na nyerere road kupitia soko la machinga complex kabla ujavuka reli utaona maduka au Maeneo hayo pinda kushoto kama unataka kuelekea kariakoo kuna maduka mengi used spares part au ata ukiuliza tu utaoneshwa wale jamaa utaona wanauza spares pia in mafundi wazuri sana na Hanna spares ambayo utakosa pale.
 
kama unakumbuka nilikwambia ogopa mafundi wa chini ya miembe...ogopa sana hao watu
 
Ukiwa umetokea buguruni Kwenye makutano ya ilala boma shuka na Barabara inayoelekea kwenda kukutana na nyerere road kupitia soko la machinga complex kabla ujavuka reli utaona maduka au Maeneo hayo pinda kushoto kama unataka kuelekea kariakoo kuna maduka mengi used spares part au ata ukiuliza tu utaoneshwa wale jamaa utaona wanauza spares pia in mafundi wazuri sana na Hanna spares ambayo utakosa pale.
Mtaa wa Lindi.
 
Mkuu Ndama 1 kama una namba za hao mafundi weka hapa maana wahitaji tuko wengi
 
Back
Top Bottom