Mrejesho: Vituo vya Mafuta vya Total na haya mafuta yao yenye kemikali ya Excellium (Total Excellium)

Mrejesho: Vituo vya Mafuta vya Total na haya mafuta yao yenye kemikali ya Excellium (Total Excellium)

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Niliona Matangazo yao kuhusiana na mafuta yenye kemikali ya Excellium.wakisema kuwa ni mafuta ambayo yanasafisha engine na kuifanya gari iwe nyepesi. lakini zaidi zaidi wamekuwa wakisema kuwa inasaidia kutumia mafuta kidogo ukilinganisha na mafuta mengine iwe ni kwenye Disel au Petrol.

kama kawaida niliamua kwanza kuingia kwenye mtandao.nikakuta ni kweli hata South Afrika wanatumia hii kemikali kwenye vituo vya Total. nikaenda kituo flan cha Total kariakoo.nikamuuliza muuzaji kuhusiana na hii kemikali.hakuwa na majibu yanayoeleweka zaidi ya kusema hafaham sana ingawa alienda training. so hakuweza kunishawishi. nikaenda kituo kingine mitaa ya karume baada tu ya mataa nikauliza nako nikakuta dada mmoja haelewi lolote kuhusiana na hii kemikali lakini wakati huo niki mhoji maswali akatokea kaka mmoja ambaye ni meneja wa hicho kituo.

huyu alisema akimsema yule dada kuwa unashindwaje kumwelekeza mteja na wakati ulienda training. akachukua jukumu la kunielezea.ikabidi nipark pembeni niache wateja wengine waendelee mimi nipate maelezo wanasema from the horse's mouth. jamaa akaelezea mengi sana ila haya ni mambo ambayo aliyagusia

1. inasafisha engine.
MIMI: hapa nilimuuliza inasafishaje? na ule uchafu baada ya kusafishwa engine unaenda wapi? maana najua unaposafisha kitu maana yake inabidi uchafu utoke.

YEYE : uchafu una dissolve humo humo.

MIMI: hapa nilipata ukakasi sana nikawaza kuwa kama nina kikombe kichafu nikaweka maji au juice ile juice ikaondoa ule uchafu ulionata pembezon ndani ya kikombe ila ukabaki humo humo nikaendelea kunywa juice je itakuwa safi?

WADAU: Nisaidieni hapa inakuaje kitaalam..mara nyingi uchafu wa engine nadhan ni some particles ambazo maybe zinasababishwa na msuguano au petrol/disel chafu.sijui nahitaj msaada

2. Inasababisha engine kuwa nyepesi

MIMI:
week nzima iliyopita nimekuwa nikiweka hayo mafuta tena baada ya kuhakikisha yale mengine nimemaliza kwenye Tank nikaamua weeke nzima niweke Total Excellium. sijaona mabadiliko. gari ipo vile vile haikuwa nzito ila sijaona mabadiliko kuwa sasa labda ingekuwa nyepes zaidi.labda sijaona mabadiliko sababu gari ilikuwa nyepesi toka mwanzo.sijui

3.inapunguza ulaji wa mafuta

YEYE:
anatumia gari ndogo ya hiace toka mbagala mpaka hapo kariakoo mafuta ya 10,000 anatumia siku mbili.

MIMI: toka kwangu mpaka kazini kwa gari yangu mafuta ya kawaida ya 15,000 natumia siku mbili bila wasiwasi na kutoka kwangu mpaka kazini kwenda na kurudi ni kms 26.

nimeweka mafuta hayo ya TOTAL EXCELLIUM ya 20,000 jumatatu nikiwa naelekea kazini lakini jana nimerudi gauge iko chini sana.sivyo nilivyotegemea kuwa angalau basi ingetumika kwa siku 3.

wadau naombeni uzoefu wenu kuhusiana na mafuta haya ya TOTAL EXCELLIUM. kama kuna namna ya kujibu hayo maswali kitaalam pia mnisaidie.ili pamoja wana genzi tuweze kujua kipi ni bora kwa matumizi ya magari yetu.
 
Mm pia niliambiwa juzi kuhusu hayo mafuta, kikawaida huwa natumia mafuta ya 120k kutoka Arusha hadi Dar, juzi nimeweka hayo mafuta, nikatumia 145K, japo alinambia effect yake nitaiona baada ya muda, ..............mwenye uthibitisho anaweza kutusaidia,.....
 
Mafuta ni yale yale hapo wameremba tu kibiashara ili waonekane watofauti, eti yame contain detergents ambayo inasafisha sensitive engine parts kama vile injectors.... LoL.
 
ndo hapo nashindwa kuelewa hata kwangu sijaona tofauti.... jamaa wasije wakawa wanatumia tu lugha ya biashara kuturubuni.

Mm pia niliambiwa juzi kuhusu hayo mafuta, kikawaida huwa natumia mafuta ya 120k kutoka Arusha hadi Dar, juzi nimeweka hayo mafuta, nikatumia 145K, japo alinambia effect yake nitaiona baada ya muda, ..............mwenye uthibitisho anaweza kutusaidia,.....
 
Ha ha ha ha biashara ya mafuta imekuwa ngumu, kila mtu anaingia humo matokeo yake watu wanakuja na ubunifu wa kuwapata wasiojiuliza maswali.

Huwa sipendi kusema biashara za watu ila mafuta hata yawe vipi mabadiliko yatakayokuletea kwenye ulaji wa mafuta ni madoooooogo sana kiasi huwezi kuona na haina maana yoyote kwa mtumiaji.
 
Changes zipo kubwa sana endapo gari lako litakua jipya...

Kama siyo jipya ili uone changes huna budi kushusha tank la mafuta na kulisafisha lote, badilisha filter, safisha pump au irekebishe kwenye standard yake... hapo ndiyo utaona changes...

Cc: mahondaw
 
1. inasafisha engine.
MIMI: hapa nilimuuliza inasafishaje? na ule uchafu baada ya kusafishwa engine unaenda wapi? maana najua unaposafisha kitu maana yake inabidi uchafu utoke.
YEYE : uchafu una dissolve humo humo ........
Mkuu hapa uchafu unauzungumzwa na ule unaosababishwa na combustion ya engine. Siku moja ukienda kufungua engin itizame ile piston ilivo nyeusi. Sifikirii kama kweli eti inasafisha, kwa sababu mafuta yanavokuwa pumped kwenye engine ni kama vapour, piston ikikaribia top end mripuko unafanyika, sasa sijui ni mda gani hio Excellium kusafisha engine.

Wala hakuna fuel efficiency yoyote ni kuwavuta wateja wowote. Unataka kusafisha engine kafanye engine flush. Au fungua engine yote ioshe kwa mafuta ya taa
 
Mie always ni GBP na Barrel. Sioni kama total wana jipya hasa ukizingatia kwa mfumo wa sasa wa uagizaji wa tenda. Hizo aftermarket additives wanaweka wapi? Reserve zao za mafuta ni safi huko chini?.

It is just another way of fishing out customers in this competitive market

Sent from my SM-J700F using Tapatalk
 
Niliona Matangazo yao kuhusiana na mafuta yenye kemikali ya Excellium.wakisema kuwa ni mafuta ambayo yanasafisha engine na kuifanya gari iwe nyepesi. lakini zaidi zaidi wamekuwa wakisema kuwa inasaidia kutumia mafuta kidogo ukilinganisha na mafuta mengine iwe ni kwenye Disel au Petrol.

kama kawaida niliamua kwanza kuingia kwenye mtandao.nikakuta ni kweli hata South Afrika wanatumia hii kemikali kwenye vituo vya Total. nikaenda kituo flan cha Total kariakoo.nikamuuliza muuzaji kuhusiana na hii kemikali.hakuwa na majibu yanayoeleweka zaidi ya kusema hafaham sana ingawa alienda training. so hakuweza kunishawishi. nikaenda kituo kingine mitaa ya karume baada tu ya mataa nikauliza nako nikakuta dada mmoja haelewi lolote kuhusiana na hii kemikali lakini wakati huo niki mhoji maswali akatokea kaka mmoja ambaye ni meneja wa hicho kituo.

huyu alisema akimsema yule dada kuwa unashindwaje kumwelekeza mteja na wakati ulienda training. akachukua jukumu la kunielezea.ikabidi nipark pembeni niache wateja wengine waendelee mimi nipate maelezo wanasema from the horse's mouth. jamaa akaelezea mengi sana ila haya ni mambo ambayo aliyagusia
1. inasafisha engine.
MIMI: hapa nilimuuliza inasafishaje? na ule uchafu baada ya kusafishwa engine unaenda wapi? maana najua unaposafisha kitu maana yake inabidi uchafu utoke.
YEYE : uchafu una dissolve humo humo ........
MIMI: hapa nilipata ukakasi sana nikawaza kuwa kama nina kikombe kichafu nikaweka maji au juice ile juice ikaondoa ule uchafu ulionata pembezon ndani ya kikombe ila ukabaki humo humo nikaendelea kunywa juice je itakuwa safi?
WADAU: Nisaidieni hapa inakuaje kitaalam..mara nyingi uchafu wa engine nadhan ni some particles ambazo maybe zinasababishwa na msuguano au petrol/disel chafu.sijui nahitaj msaada

2. Inasababisha engine kuwa nyepesi....
MIMI:
week nzima iliyopita nimekuwa nikiweka hayo mafuta tena baada ya kuhakikisha yale mengine nimemaliza kwenye Tank nikaamua weeke nzima niweke Total Excellium. sijaona mabadiliko. gari ipo vile vile haikuwa nzito ila sijaona mabadiliko kuwa sasa labda ingekuwa nyepes zaidi.labda sijaona mabadiliko sababu gari ilikuwa nyepesi toka mwanzo.sijui

3.inapunguza ulaji wa mafuta
YEYE:
anatumia gari ndogo ya hiace toka mbagala mpaka hapo kariakoo mafuta ya 10,000 anatumia siku mbili
MIMI: toka kwangu mpaka kazini kwa gari yangu mafuta ya kawaida ya 15,000 natumia siku mbili bila wasiwasi na kutoka kwangu mpaka kazini kwenda na kurudi ni kms 26.
nimeweka mafuta hayo ya TOTAL EXCELLIUM ya 20,000 jumatatu nikiwa naelekea kazini lakini jana nimerudi gauge iko chini sana.sivyo nilivyotegemea kuwa angalau basi ingetumika kwa siku 3.

wadau naombeni uzoefu wenu kuhusiana na mafuta haya ya TOTAL EXCELLIUM. kama kuna namna ya kujibu hayo maswali kitaalam pia mnisaidie.ili pamoja wana genzi tuweze kujua kipi ni bora kwa matumizi ya magari yetu.
Mkuu Gu Dume kwanza pole kwa yaliyokukuta. Mimi ni mdau wa Total na nitakusaidia.
  1. Kwanza, mafuta yote Tanzania yanaletwa na muagizaji wa pamoja, bulk procurement, lakini yakifika, baadhi ya makampuni yanayafanyia treatments kwa ku add, addictives, ni viambata.
  2. Total wao wana add kiambata cha Exellium, kiambata hiki husaidia kusafisha engine ya gari kadri unavyokwenda kilometre hadi kilometre, unatumia mafuta kidogo na unakwenda mwendo mrefu huku gari yako ikiwa nyepesi.
  3. Gari inapokwenda, engine inachoma mafuta, combustion kule kwenye piston chambers, by products za hiyo combustion ni hewa ya carbon dioxide, yaani hewa ukaa, ambayo ndio inatoka nje kwa kutumia exhaust pipe, bomba la moshi.
  4. Ule moshi wa gari, una contains carbon particles, masizi, hayo masizi, yanatoka kwenye engine, masizi hayo yakuzudi, ile combustion inasababisha corrosion, yaani engine yako inakuwa corroded na carbon particles, na hizo carbon particles zinapotoka kwa nguvu kwenye emissions process zinakula kuta za piston na kuchakaza piston rings na hadi kutoboa exhaust pipes.
  5. Kiambata cha Exellium kinasafisha engine ya gari yako kilometre kwa kilometre kwanza kwa kuyachoma mafuta yote, hakuna carbon particles za kuchakaza engine na gari inatoa moshi mweupe msafi, na sio moshi mweusi, mchafu.
  6. Engine inapokuwa safi, inachoma mafuta kidogo na kwenda umbali mrefu huku inadumu, na kudumu na kudumu zaidi
  7. Angalizo: ili ufaidi haswa manufaa ya Total Exellium, lazima engine ya gari yako iwe ni hizi engine za magari ya kisasa zinazotumia premium fuels, gari yako kama ni ya zamani, na engine za ngwalangwala, you can't notice the difference.
  8. Na katika fuels efficiency, huwezi kuipima kwa kujaza mafuta ya elfu 20,000 kama mtu wa boda boda, lazima ujaze full tank kwa mafuta ya kawaida, take note ya kilometres uangalie hiyo full tank utakwenda kilometres ngapi, note down. Kisha jaza full tank mafuta ya Total Exellium, angalia utakwenda kilometres ngapi!.
  9. Amini nakuambia, kama gari yako ni ya kisasa, ukiisha onja Total Exellium, hutakaa urudie mafuta ya kawaida, unless kama wewe ni mwenzangu na mimi wale wa uchumi wa kijungu jiko na mafuta ya vidumu, endelea kujazia mafuta kituo cha karibu yako.
  10. Kama una muda, wasikize hawa madereva
Jee Kuna Ukweli Kuwa in Tanzania, Mafuta ya Vituo vya Total, " They are The Best?. If Yes, How Wakati Tunanunua Bulk?.

P
 
Mkuu Gu Dume kwanza pole kwa yaliyokukuta. Mimi ni mdau wa Total na nitakusaidia.
  1. Kwanza, mafuta yote Tanzania yanaletwa na muagizaji wa pamoja, bulk procurement, lakini yakifika, baadhi ya makampuni yanayafanyia treatments kwa ku add, addictives, ni viambata...
  1. Wenye Share zao,,

Sawa Anko wa Mkwepu,,[emoji120]
 
Mkuu Gu Dume kwanza pole kwa yaliyokukuta. Mimi ni mdau wa Total na nitakusaidia.
  1. Kwanza, mafuta yote Tanzania yanaletwa na muagizaji wa pamoja, bulk procurement, lakini yakifika, baadhi ya makampuni yanayafanyia treatments kwa ku add, addictives, ni viambata...
Pascal Mayalla kwann walikunyima ubunge?

Maana Kwa madini uliyonayo kichwani huko bungeni kungenoga kwelikweli
 
😂😂😂😂😂 gari yangu halikuwa toleo jipya sana
Ni la zamani toleo la mwaka 2014 na mimi nlinunua mwaka 2017. Miaka 3 baadaye. Likiwa limetembea kms 24,000 toka liuzwe kwangu.

Miaka yangu yote ya matumizi ya magari toka kipindi hicho cha early 2000. Nlikuwa naheshiku Makampuni ya BP,Total, Gapco, miaka ya nyuma nakumbuka mzee alikuwa anapenda sana kununua Shell.

Anyway...mimi niheshimu mawazo yako.

Mkuu Gu Dume kwanza pole kwa yaliyokukuta. Mimi ni mdau wa Total na nitakusaidia.
  1. Kwanza, mafuta yote Tanzania yanaletwa na muagizaji wa pamoja, bulk procurement, lakini yakifika, baadhi ya makampuni yanayafanyia treatments kwa ku add, addictives, ni viambata...
 
😂😂😂😂😂 gari yangu halikuwa toleo jipya sana
Ni la zamani toleo la mwaka 2014 na mimi nlinunua mwaka 2017. Miaka 3 baadaye. Likiwa limetembea kms 24,000 toka liuzwe kwangu. Miaka yangu yote ya matumizi ya magari toka kipindi hicho cha early 2000. Nlikuwa naheshiku Makampuni ya BP,Total, Gapco, miaka ya nyuma nakumbuka mzee alikuwa anapenda sana kununua Shell.

Anyway...mimi niheshimu mawazo yako.
Gari la 2014 ni gari jipya. Jaza full tank mafuta ya kawaida, hesabu kilometres, then jaza Exellium,linganisha, come back utaniambia.
P
 
Mkuu Gu Dume kwanza pole kwa yaliyokukuta. Mimi ni mdau wa Total na nitakusaidia.
  1. Kwanza, mafuta yote Tanzania yanaletwa na muagizaji wa pamoja, bulk procurement, lakini yakifika, baadhi ya makampuni yanayafanyia treatments kwa ku add, addictives, ni viambata....
  1. Hii Sad News Vp Tena Anko,[emoji1745]
    Screenshot_20200903-090845_WhatsApp.jpg
 
Back
Top Bottom