Mrejesho wa mwezi mmoja baada ya kuacha kazi

Jenseny

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2011
Posts
1,743
Reaction score
1,738
Ref my previous post

Namshukuru mwenyezi Mungu muumba wq mbingu na ardhi kwa pumzi na afya njema aliyonijaalia

ilinichukua miaka mitano na nusu kuacha kazi ya serikalini nashukuru Mungu kwa walionisupport juu ya uamuzi wangu huo

nliwakwepa wale wote ambao nlihic watanikatisha tamaa hasa wazazi wangu ilibidi nimtengenezee mazingira ya kutokuniomba hela ya kila mwezi kwa kumwekea pooltable linalomwingizia 150000 kila mwezi

Ninachofanya baada ya kuacha kazi

Ninalima matikiti maji,Zukini na pilipili za kuwasha nimeanza na tikiti maji heka 3 pilipili za kuwasha nusu heka na zukini nusu heka

Zukini na pilipili ndo zao ninalolitegemea kulifanya liwe zao la biashara nimelilima chache kwasababu ckuwahi kulima zukini na pilipili so natafuta experience

tikiti ziko poa ntawaonyesha picha za zilipofikia

Biashara

nimefanya biashara ya mbolea ya mavi ya kuku kwa muda wa week 2 nimeingiza faida ya laki4 though changamoto imekuja kwenye savings kila nkipata hela mahitaji ya shamba yanaongezeka mf dawa mbolea ya dukani kuwalipa posho vibarua nk

Uzuri wa kujiajiri

unaamua ufanye nini muda gani mwenyewe yaani kama nkiamua nisafiri hata nw naweka mipango sawa naenda popote inshort nipo huru

changamoto kuubwa nliyoiona

Savings na mifuko ya jamii

faida inapaswa ihifadhiwe kiac kikubwa kuliko kukitumia mara nyngi tunatumia hela pale tunapokua nazo tusipokua nazo ni ngumu sana kuzitumia natamani nijifunze mbinu ya kisave

natamani nijiunge na ule mfuko binafsi wa penshen tatizo huku Jaribu(kibiti) hakuna hicho kitu

View attachment 848013View attachment 848015

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera mkuu na kila la kheri. Kuhusu kusave kwenda hatua kwa hatua hata kama utaanza kusave kiasi kidogo baada ya kununua madawa/mbegu because that’s still an investment over the investment
 
Hongera sana kwa maamuzi hayo kila la Kheri
 
Hapo kwenye kusave boss unahitaji mwanamke mwenye akili, watu wengine tuna wanawake wako bright sana kwenye maswala ya uchumi ingawa darasani hawajaingia ila wanaume ndiyo makopo yanayokwamisha mambo.

Hata nahisi nampotezea muda wake tu.
 
Safi sana usife moyo kaza buti tu mpaka kitaeleweka mkuu
 
Hongera kwa maamuzi ya kijasiri. Keep it up!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…