Mrejesho wa mwezi mmoja baada ya kuacha kazi

Zabibu imekosa soko wakulima wanalia! Hizi ni changamoto katika uzalishaji muhimu kuchunguza soko Kabla ya kuwekeza!
Soko limeyumba sana
Soko Soko Soko......
 
Hongera sana mkuu kwa huo UJASIRI maana kuajiriwa kunazalisha uoga wa hali ya juu

Halafu umechagua mazao exclusive inaonesha ulijipanga.
 
Huu ujasiri nauvutia pumzi sana,time will tell,haiwezekani 5yrs mshahara hata mia hauongezeki,cheo kile kile,matamko kila uchwao,HONGERA MKUU NA MUNGU AKUONGOZE BAADA YA UAMUZI HUO
 
Huu ushauri kwa mtu unayetaka kuacha kazi usichukue...hawa ndo wanaowapa uoga wenzao huko maofisini...nilishapitia situation kama hii na bahati mbaya wengi ya watu waliokua wamenizunguka ni kama huyu nilichukua maamuzi magumu na bahati nzuri nimefanikiwa kwa hichi kidogo nipatacho...wale waliokuwa wananipa uoga ndo hao ckuhz wananipigia simu eti niwashauri namna ya kuchomoka kule..za kuambiwa changanya na zako..cha msingi kila mmoja afanye moyo wake unachomtuma
 
Mkuu ni wangapi waliofanya kama wewe wakafanikiwa?? Akili za kuambiwa hizi.
 
Hongera kwa kusoma nyakati..kwa huu mwendo wa jiwe, mtumishi wa serikali asitegemee kutoboa zaidi kama hatajiwekeza ktk ujasiriamali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli Mkuu,hapa ni kutimiza ya serikali huku ukididimia kimalengo na kiuchumi,na siku hizi hata kiinua mgongo ni Ishu na ile formula mpya ya mifuko ya hifadhi ni kilio [emoji23] [emoji23]
 
Pia kusema hivyo haimaanishi kumkatisha mtu tamaa bali kumsaidia the risk around ili azipunguze inapobidi. Mtoa uzi mwenyewe kasema alimnunulia Baba yake pool table kabla ya kuacha kazi.
 
Mkuu ni wangapi waliofanya kama wewe wakafanikiwa?? Akili za kuambiwa hizi.
Kwani wangapi ambao wapo kwenye hizo ajira wamefanikiwa????..mbona hata waliopo kwenye hizo ajira wanalia tu njaa...cha msingi kila mtu afuate moyo wake unachomtuma afanye lakini tusitishianetishiane.
 
Hongera sana Mkuu.Inshallah njia iwe nyeupe katika mafanikio yako.
 
Kwani wangapi ambao wapo kwenye hizo ajira wamefanikiwa????..mbona hata waliopo kwenye hizo ajira wanalia tu njaa...cha msingi kila mtu afuate moyo wake unachomtuma afanye lakini tusitishianetishiane.
Kilio cha wenye ajira ni tofauti kabisa na cha wasio na ajira au waliojiajili. Kufata moyo wako bila risk assessment ni hatari. Nadhani kila mtu apime uwezo wake wa kuhimili hiyo risk ikitokea mambo yakagoma. Halafu dhana ya kusema kuajiliwa ni kubaya si nzuri, maana ukijiali nawe utahitaji kuajili watu, sasa kama wote wakichukia kuajiliwa itakuwaje. Mwisho si kwamba kupitia ajira huwezi fanikiwa ni mahesabu tu.
 
Pia kusema hivyo haimaanishi kumkatisha mtu tamaa bali kumsaidia the risk around ili azipunguze inapobidi. Mtoa uzi mwenyewe kasema alimnunulia Baba yake pool table kabla ya kuacha kazi.
Maneno aliyoongea ndo hayohayo wanayoongea huko maofisini wakiona mwenzao anataka kuachana na kuajiriwa ili kukatishana tamaa...kila mtu anapofanya maamuzi lazima kuna vitu anakuwa amejipanga
 
Wenye ajira unaowazungumzia wewe ni wapi...hawa ma teacher wanaolipwa laki tatu????
 
Maneno aliyoongea ndo hayohayo wanayoongea huko maofisini wakiona mwenzao anataka kuachana na kuajiriwa ili kukatishana tamaa...kila mtu anapofanya maamuzi lazima kuna vitu anakuwa amejipanga
Anhaaa kumbe hadi ujipange? Si uache tu, sasa kwa nini husisitizi vitu gani mtu ajipange kwanza? Ingekuwa vizuri ukajikita zaidi kwenye kufundisha vitu vya kujipanga kabla ya kuacha.
 
Anhaaa kumbe hadi ujipange? Si uache tu, sasa kwa nini husisitizi vitu gani mtu ajipange kwanza? Ingekuwa vizuri ukajikita zaidi kwenye kufundisha vitu vya kujipanga kabla ya kuacha.
Hamna mtu anayeacha kazi then hajui na hajafanya mipango ya kesho yake...kila mtu anaacha na kichwani mwake anajua anaenda kufanya nini...nachopinga mimi ni mtu yupo kwenye ajira then anampa ushauri mtu anayeacha kazi na anamshauri eti aanzishe mradi wakati yupo kwenye ajira ili mradi ukikua ndo aache kazi wakati huohuo huyo anayetoa ushauri na yupo kwenye ajira hana mradi hata wa kufuga kuku wawili....unanishauri vipi mimi namna ya kupata mafanikio wakati we we hunabhayo mafanikio...or wewe hupendi mafanikio...maswali yangu ndo huwa yapo hapo
 
Ajira rasimi yoyote.
Kama ndo hao tunaishi nao huku mtaani usituambie chochote kuhusu wao...tunawaona kwa macho yetu...alafu wengine tushapitia huko kwa hiyo tunajua kila kitu...na si kwamba huku tulipo kuna maisha mazuri hakuna...but tunaiona tofauti...cha msingi naendelea kusisitiza kila mtu afanye moyo wake unachopenda...
 
Wewe hujaacha kazi mkuu umebadilisha kazi kutoka Kuajiriwa na kujiajiri,kazi yako ili ikukomboe kiuchumi unatakiwa ufikie kiwango cha kuwa na watu uliwaajiri kisha wakuletee pesa zaidi sana ni namna ya kufanya kutengeneza channel ili pesa zikufuate wewe nasio sio viceversa hapo ndio tutasema kuwa ajira binafsi imekukomboa wala haitakiwi iwe ni msuguano mkali wa harakati za kutafuta pesa ili ulipie wage bills za na manpower yako katika phase ya mwanzo ya kujenga uchumi ni ngumu sana lakini ikifanikiwa kuweka mifumo na kuisimamia phase ya pili ni Monitoring na phase ya tatu ndio harvesting kila na kupata returns ambazo zitakufanya hata wakati unarudi kwenye kazi yako ya kilimo basi hata income yako kutoka vyanzo vyako ikusaidie usistruggle sana kuendesha kilimo chako.Ukiona vipi unaweza kubadilisha diversify mtaji wako kutoka kwenye ukulima ukawa mtu kununua na kuuza mazao,hapo itakupunguzia charges nyingi za kulipa watu wengi na faida yako itategemea nguvu ya soko.Wanaokimbia kilimo na gharama zake za uendeshaji wanapata faida mara3 zaidi ya kuwa wakulima na wauzaji wa mazao yao wao wenyewe.
Nikutakie Harakati njema sana za kujikomboa Kiuchumi Direction ndio msingi wa ustawi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…