Mrema awatuhumu wajumbe kugeuza Bunge ‘shamba’ la Bibi!

Mrema awatuhumu wajumbe kugeuza Bunge ‘shamba’ la Bibi!

makoye2009

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Posts
2,638
Reaction score
1,218
Dodoma. Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Augustine Mrema amedai baadhi ya wajumbe wanataka kuligeuza bunge hilo ‘shamba la bibi' kwa kudai posho zaidi kwa kisingizio cha kupanda gharama za maisha.

Akizungumza mjini hapa jana, Mrema alisema wajumbe wanaoshawishi wenzao kudai posho zaidi ni wale waliopelekwa kuishi kwenye hoteli za bei ya juu kati ya Sh100,000 na Sh220,000 kwa siku.

Mrema alisema Sh300,000 wanacholipwa kinatosha kwa sababu kuna hoteli nzuri za kati ya Sh15,000 hadi Sh40,000, ambazo zina hadhi na sifa ya kuishi wajumbe wa Bunge la Katiba.

"Mjumbe ameamua kwenda kuishi chumba cha Sh200,000 wakati akijua atalipwa Sh300,000 halafu analalamika kupanda kwa gharama za maisha… hizi gharama zimetengenezwa,"alisema Mrema.

Alitaka kamati ya watu sita iliyoundwa na Bunge kufuatilia suala la posho, ifanye uchunguzi nyumba za kulala wageni walizofikia wajumbe kubaini ukweli wa kupanda kwa gharama.

Mrema alisema nyumba nyingi za kulala wageni ikiwamo yake haikuorodheshwa kwenye hoteli walizopewa wajumbe.

"Mimi hapa kwangu vyumba vinaanzia Sh20,000, bado tunaweza kuzungumza lakini haikuingizwa kwenye orodha… nakwambia huu ni mchongo ili wajumbe waende nyumba fulani-fulani," alisema Mrema na kuongeza:

"Ughali wa maisha unatengenezwa, zipo tupu na watu wamekimbilia hizo za ghali ili waje wadai posho zaidi… Hayo ni matakwa kama wanataka waje huku kwangu maisha ni bwerere wasitake kuingiza Serikali gharama."

Alihoji sababu za wajumbe hao pekee kupiga kelele za kuongeza posho, ilhali kuna makundi mengine yanayofanya kazi hizohizo.

Source: Mwananchi newspaper

My take: Mzee wa Kiraracha umenena vema. Kumbe bado unaonekana kuwa na busara na hikma na umenikumbusha zile enzi zako ulipokuwa N/Waziri Mkuu ukitoa amri za siku 7 kwa majambazi na vibaka kusalimisha silaha zao. Hongera sana akwi. Tunataka Wabunge wengine wa Bunge la Katiba hasa wale wa CCM waige mfano wako na wawe na mtazamo kama wa kwako ili hatimaye muweze kutimiza adhima na malengo yaliyowapeleka Dodoma ambayo ni ya kuwatengenezea Watanzania Katiba mpya.
 
Wana jf niko dodoma na nimepata bahati ya kuzungumza na baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba nikapa dokezi kuwa walio wengi wamepanga room na kulipa kodi ya elfu 30 kwa mwezi na na wengine wamelipa kodi ya elfu 50 kwa mwezi inategemeana na uzuri wa chumba anacho panga na inasemekana waliopanga wameweza kulipa cash kwa miezi mitatu ambayo waliyo lipishwa elfu 30 wameweza lipa elfu 90 kwa miezi mitatu.
Nikaona kama watawezafanya hivyo waliyo wengi watarudi makwao na pesa nyingi sana ambazo watakwenda kuanzisha biashara au kufanyia mambo ya maana
Pia wana paswa kumshukuru mtu aliye leta hoja ya uwanzishwaji wa katiba mpya kwa sababu imeweza kuwa faida kwao.
 
huyu mbunge wangu nampenda sana kaongea point..... na kuna wengine nasikia wamechukua vyumba viewili ili awe anawaalika ndugu jamaana rafiki
 
Safi sana unajua wakijibana ivo wataondoka na hela ndefu na kuanzisha tumiradi tya maana tu!
 
Wanataka pesa za viburudisho laki 3 nyingi sana kwa siku. Kima cha chin mshahara kwa mwez haifiki laki ata laki 2
 
katuni-nipashe-bonge-la-katiba-100214.jpg
 
Back
Top Bottom