Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,860
Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema amesema watu wanaotaka kura ya siri bungeni ni wanafiki huku Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira akiahidi kuonyesha wazi msimamo wake na kwamba ukiathiri ustawi wa taifa anataka aadhibiwe angali hai au mfu.
Wakizungumza kwenye mahojiano na televisheni ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jana, Mrema na Wassira walisema wao wanataka kuonyesha msimamo wao.
Mrema alisema wajumbe wanaotaka kura ya wazi kwa kisingizio cha kuhofia kushughulikiwa na vyama vyao ni wanafiki na kuwataka waige mfano wake.
Naye Wasira alisema hakuna sababu inayoweza kuhalalisha kura ya siri katika kuamua mambo nyeti ya kitaifa kama kuunda na kupitisha Katiba Mpya.
Alisema kama ni suala la msimamo wa mtu kutofautiana na ule wa chama au kundi lililomweka kwenye nafasi hiyo, utafahamika kupitia kwenye mijadala yake, ndani ya Bunge, Kamati au katika mazungumzo yake ya kawaida.
Mimi msimamo wangu ni serikali mbili kwa sababu ni wenye historia inayoeleweka kuwa una dhamira ya kuunda mfumo wa muungano endelevu na nyingine nyingi zilizo njema kwa watu wote, nitasimamia msimamo huo na ikitokea ukaleta madhara kwa taifa, hata nikishakufa watoto na wajukuu wangu waje tu kwenye kaburi langu, wanichape viboko, alieleza Wassira.
Mrema alisema alikuwa waziri akaweka wazi msimamo wake uliokuwa kinyume na chama chake wakati huo (CCM).
Kila mtu anafahamu yaliyonikuta, hadi leo yapata miaka 20 sijalipwa mafao yangu. Wananchi wangu si wamenirudisha bungeni? Anayeficha msimamo wake ni mnafiki, wala hafai kuwa kiongozi, alieleza Mrema, ambaye alitimuliwa uwaziri mwaka 1994.