Mrema sasa ni Daktari?

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Nimesikia jana RFA wakisema mbunge wa Vunjo DR. Augustine Lyatonga Mrema amfagilia Kikwete ndio nikastuka kwani sikuwa najua kuwa jamaa kasha ukwaa udokta. Sasa sijajua kama ni wa kusoma na kufanya utafiti au ni wa kupewa na kama kapewa ni chuo gani kimempa? Hongera Dr. Augustine Mrema maana zamani walikuwa wanasema huna elimu ya kutosha. Kitu kingine nilichojifunza ni kuwa kwenye siasa hakuna uadui au urafiki wa kudumu. Huyu huyu Mrema alikuwa anamponda Kikwete kuwa hawezi kuongoza kwakuwa hajawahi hata kuchaguliwa kuwa mjumbe wa nyumba kumi lakini leo anamfagilia. Ndivyo tukavyoshuhudia kwa kina Zitto na Mwigamba wakigeuka na kuisifu CCM
 
Nimesoma na Mimi leo gazeti la Majira ukurasa wa tatu , iwekwe sawa hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…