MRI ipo Temeke referral hospital?

MRI ipo Temeke referral hospital?

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,266
Reaction score
3,698
Wakuu nauliza kwenu tena hivi Temeke hospital kuna kipimo cha MRI?

NIna mgonjwa wangu anaumwa kichwa sanaa hawezi kuongea Wala kutembea vizurI.

Alianza kuumwa kifua anakohoa sana mpaka damu akawa hawezi hata kula, baadae akaja kupoteza fahamu.

Tukamleta hapa Temeke kapimwa wanasema ana amoeba/minyoo,na madonda ya tumbo wampima kwa damu wanasema anayo.

Mpaka sasa ana wiki mbili hali yake bado sio nzuri.

Msaada wenu wa mawazo mgonjwa wangu atakua na ugonjwa gani hasa.

Vipi je ninaweza omba refaral nikapewa kwenda Muhimbili?
 
Pole sana,

1: Temeke RRH, hawana MRI bali wana CT scan. Ila suala la msingi ni kujua ni kipimo kipi kinahitajika kulingana na tatizo la mgonjwa.

2: Unaweza kuomba referral kwenda Muhimbili, ni kujenga hoja tu.

3: Ni vyema pia kuwasiliana vyema na daktari anaemhudumia mgonjwa ili kujua/kuelewa zaidi:
A: Tatizo la msingi la mgonjwa kulingana na malalamiko mengine.
B: Mtizamo wa vipimo zaidi kwa mgonjwa.
B: Mwendelezo wa tiba ya mgonjwa husika.
 
Mwenenendo wa tiba kwa mgonjwa Hali yake Bado Iko pale pale...wanasema amoeba ndo umemfanya aumwe sana Hadi kichwa nakutaka kuvimba kichwa kwamba minyoo imeingia ktk mfumo wa damu
 
Kuna maelezo unayoyatoa, yanaonyesha hamjasikilizana vyema na daktari.

1: Amoeba si minyoo, hivyo nadhani kuna mambo yanachanganywa.

2: Kama wameweza kuona minyoo kwenye damu au sehemu nyingine ya mwili zaidi ya njia ya chakula, maana yake kuna vipimo vingine vimefanyika.

3: tukizungumzia mwenendo wa tiba, inajumuisha:
A: Mawazi ya daktari juu ya vipimo zaidi
B: Dawa
C: Mtizamo wa mgonjwa kurejea vyema/prognosis, kulingana na hali yake.

Hii itakusaidi kwa chochote itakachofikiria juu ya mgonjwa.
 
Mwenenendo wa tiba kwa mgonjwa Hali yake Bado Iko pale pale...wanasema amoeba ndo umemfanya aumwe sana Hadi kichwa nakutaka kuvimba kichwa kwamba minyoo imeingia ktk mfumo wa damu
Pole sana mgongjwa amekuja kupona?
 
Back
Top Bottom