Mrisho Gambo ageuka mbogo kusuasua kwa ujenzi wa barabara ya Engosheratoni jijini Arusha

Mrisho Gambo ageuka mbogo kusuasua kwa ujenzi wa barabara ya Engosheratoni jijini Arusha

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mrisho Gambo, ametembelea mradi wa ujenzi wa Barabara ya Engosheraton jijini Arusha na kumtaka mkandarasi wa mradi huo, Jiangxi GEO, kuongeza kasi ya utekelezaji.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Gambo amesema barabara hiyo ilitakiwa kuwa imefikia asilimia 86 ya utekelezaji, lakini hadi sasa imefikia asilimia 60 pekee, kwa mujibu wa wasimamizi wa mradi.

Mkandarasi huyo amekiri kuchelewa kupeleka mitambo kwa karibu wiki tatu na ameahidi kuanza kupeleka mitambo yote inayohitajika kuanzia kesho.

Aidha, amesisitiza kuwa miradi ya miundombinu inapaswa kusimamiwa kwa ufanisi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa wakati.


 
Huko ni kutapatapa kwa Mwana Ilala Boma..too late..ni bora ujikite kwenye biashara zako na rafikio Mbise..wenye wapiga kura ni Madiwani na Wenyeviti wa Mitaa..sasa wengi wao wewe huelewani nao..UTATOBOA kweli??
 
Back
Top Bottom