Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mrisho Gambo akichangia Bungeni kwenye Bajeti iliyopendekezwa, ameielezea kutotoa ahueni yoyote kwenye sekta ya utalii iliyoyumba kutokana changamoto za ugonjwa wa Covid.
Amesema mchango wa utalii umeshuka kutoka asilimia 17.5 mpaka asilimia 10.7 na mapato yamepungua kutoka bilioni 584 mpaka bilioni 89 kulingana na taarifa ya wizara.
Amesema changamoto kubwa zimejitokeza hasa kwenye ajira akitolea mfano Arusha mahoteli mengi yameathirika, tour operators, waongoza watalii, madereva, wapagazi, wapiga mahema na staff wa maofisini wako hoi.
Gambo amesema pamoja na matatizo yote hayo, wizara ya maliasili na utalii na serikali imekuja na suluhisho la kuongeza tozo.
Gambo amesisitaza wizara ya maliasili na Utalii wasipoangaliwa wanaenda kuiua sekta na ameiita ni corona na mbili nchini.
Ameshauri Tozo husika zisitishwe.