Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo amesema Chama cha Mapinduzi na wanachama wake wameshafanya maamuzi ya kumteua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea wa Urais hivyo wanaopiga kelele wanapaswa kukaa kimya kwa sababu wao sio wanachama wa Chama hicho.
Gambo ameyasema hayo leo tarehe 19 Februari, 2025 Jijini Arusha wakati wa hafla ya Uhamasishaji wa kutoa Elimu ya Nishati Safi kwa Viongozi wa Baraza la Wazee Arusha ambapo anatumia fursa hiyo kueleza mafanikio na utekelezaji wa miradi ya Maendeleo Jimbo la Arusha Mjini