Uchaguzi 2020 Mrisho Gambo kuangukia pua asubuhi na mapema

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Wakuu heshima sana.

Leo niliamua kufanya tathmini yangu isiyozingatia vigezo wala kibali kutoka mamlaka husika.

Nimefanya mahojiano na makundi mbali mbali na sehemu tofauti tofauti katika viunga vya Jiji la Arusha lilotamalaki kwa uchafu na magenge yanayozua magari kupita kwa urahisi.

Ni hivi Gambo anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa waliokuwa washindani wake ndani ya CCM ambao wanafikiri chama kilishindwa kusimama katika haki na hasa suala la RUSHWA.

Wagombea wengi wameiona kamati kuu na Halmashauri kuu Taifa imeshindwa kusimamia misingi ya chama. Gambo alitumia muda mwingi katika nafasi ya RC kujijenga yeye binanafsi na si kujenga chama.

Bwana Gambo aliunda team yake ya ushindi huku akiwaengua viongozi rasmi wa chama.

Bwana Gambo alizoea kutumia madaraka ya RC kufanikisha mambo yake binafsi.Aliwanunua madiwani wa upinzani na wengine walipewa ahadi kusaidiwa kugombea ubunge ajabu alikuwa mtu wa kwanza kuchukua form ya kuwaacha Bwana Kalist wakishangaa.

Mgombea wa CHADEMA Bwana Goddess Lema sasa anaungwa mkono na wana CCM wengi tena bila kificho.
 
Mkuu tukutane 30 keshokutwa viwanja vya Relini G LEMA ataunguruma
 
Baada ya lissu kutia aibu mbagala mmekuja na ingine aya tusubiri hio kampeni, kaa ukijua huu ndo muhula wa mwisho wa lema, hakuna namna yoyote atapita tena juzi kwenye form alikua anajikomba sana ccm Mara aombe picha hio ndo news
 
Usihitimishe hivyo mkuu,lolote laweza kutokea.
 
Mkuu samahani unakaa arusha sehemu gani.... Lema anahali mbaya sana ushawishi wake umepungua sana...
Jaribu kupita kwenye masoko yote makubwa mostly samunge, kilombero na soko kuu.
Pia maeneo ya olasiti, kata ya murieti ndo utajua kwamba lema anahali mbaya
 
Wakuu heshima sana.

Leo niliamua kufanya tathmini yangu isiyozingatia vigezo wala kibali kutoka mamlaka husika.

Nimefanya mahojiano na makundi mbali mbali na sehemu tofauti tofauti katika viunga vya Jiji la Arusha lilotamalaki kwa uchafu na magenge yanayozua magari kupita kwa urahisi.

Ni hivi Gambo anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa waliokuwa washindani wake ndani ya CCM ambao wanafikiri chama kilishindwa kusimama katika haki na hasa suala la RUSHWA.

Wagombea wengi wameiona kamati kuu na Halmashauri kuu Taifa imeshindwa kusimamia misingi ya chama. Gambo alitumia muda mwingi katika nafasi ya RC kujijenga yeye binanafsi na si kujenga chama.

Bwana Gambo aliunda team yake ya ushindi huku akiwaengua viongozi rasmi wa chama.

Bwana Gambo alizoea kutumia madaraka ya RC kufanikisha mambo yake binafsi.Aliwanunua madiwani wa upinzani na wengine walipewa ahadi kusaidiwa kugombea ubunge ajabu alikuwa mtu wa kwanza kuchukua form ya kuwaacha Bwana Kalist wakishangaa.

Mgombea wa CHADEMA Bwana Goddess Lema sasa anaungwa mkono na wana CCM wengi tena bila kificho.
Badili heading yako mkuu. Bora useme uchaguz wa arusha utakuwa mgumu ila sio kumake conclusion
 
Kwenye siasa huwezi kuweka hitimisho la aina hiyo,tabia za wapiga kura huwa zinabadilika kwa dakika moja tu
 
Baada ya lissu kutia aibu mbagala mmekuja na ingine aya tusubiri hio kampeni, kaa ukijua huu ndo muhula wa mwisho wa lema, hakuna namna yoyote atapita tena juzi kwenye form alikua anajikomba sana ccm Mara aombe picha hio ndo news
Ni baada ya kuwatimuwa TBCCCM mbagala Zakheim.
 
Mkuu samahani unakaa arusha sehemu gani.... Lema anahali mbaya sana ushawishi wake umepungua sana...
Jaribu kupita kwenye masoko yote makubwa mostly samunge, kilombero na soko kuu.
Pia maeneo ya olasiti, kata ya murieti ndo utajua kwamba lema anahali mbaya
Inawezekana Lema hana ushawishi km mwamnzo,sawa, ss tatizo linakuja kwa candidate mliyemchagua kushindana nae,hili ndo tatizo!

JESUS IS LORD[emoji120]
 
Kwenye siasa huwezi kuweka hitimisho la aina hiyo,tabia za wapiga kura huwa zinabadilika kwa dakika moja tu
Sina shaka na mleta mada, ni mchambuzi mzuri wa siasa za Arusha tangu Lema alivyogombea ubunge kupitia TLP.

Thread yake ina credibility hapa jukwaani kwa sisi wakongwe tunaowajuwa vyema members wengi wa JF.
 
Lema ana kibarua kigumu sana, hata wagombea wake wa udiwani pia wana kibarua kizito.
 
Gambo anaonekana ana hofu sana, hajiamini, anajua mtihani ulioko mbele yake ni mkubwa sana kwake, ndio maana Lema alioneaha kuwa tayari kukabiliana na mgombea yeyote ambaye angepitishwa na CCM, na zaidi akasema ikibidi watia nia wote wa CCM waunganishwe ndio washindane nae Lema.
 
Kwenye siasa huwezi kuweka hitimisho la aina hiyo,tabia za wapiga kura huwa zinabadilika kwa dakika moja tu
Bahati mbaya sana tabia za wapiga kura wa arusha huwa hazibadiliki,hawaendi kwenye kampeni,hawasikilizi sera,wala hawataki kumjua mgombea!! Wao wanajua tu kupigia kura upinzani!!yaani maamuzi wanakuwa nayo kwenye macho na vidole vilivyoshika kalamu ya kutiki sehemu husika tu,kumbuka kuwa mara ya mwisho mgombea ubunge wa ccm alishinda arusha kihalali ilikuwa ni enzi ya kanali Kinana!! Tokea hapo hakujawahi kuwa na mbunge halali wa ccm arusha!! Na tatizo la ccm arusha wala si vyama pinzani,bali ccm wenyewe!!felix mrema alimhujumu Batilda buriani mchana kweupe,leo wagombea wa ccm waliokatwa wapo upande tofauti na mgombea wao,hawataki hata kumsikia!!unadhani kuna ushindi hapo? Labda kwa wizi.
 
Gambo anaonekana ana hofu sana, hajiamini, anajua mtihani ulioko mbele yake ni mkubwa sana kwake, ndio maana Lema alioneaha kuwa tayari kukabiliana na mgombea yeyote ambaye angepitishwa na CCM, na zaidi akasema ikibidi watia nia wote wa CCM waunganishwe ndio washindane nae Lema.
Endelea kujidanganya kama ww ni mkazi wa arusha you could hesitate kuongea unachosema.. lema asibweteke mvuto wake na wachadema kwa ujumla arusha mjini umepoa kinyama... October sio mbali ila mark my worda lema hashind arusha mjin this tym
 
Back
Top Bottom